Diwani wa Kata ya Namawala wilayani Kilombero, Godfrey Luena (CHADEMA) ameuawa usiku huu nyumbani kwake kwa kukatwakatwa kwa mapanga na watu wasiojulikana.


Taarifa zilizothibitishwa na mbunge wa jimbo la Mrimba kupitia chama cha Demokrasia ma Maendeleo(CHADEMA) Mhe.Suzan Kiwanga zinaeleza kuwa diwani wa kata ya Namwawala kupitia Chadema ndugu.Godfrey Luena ameuwawa kwa kukatwakatwa na watu wasiojulikana usiku huu mara baada ya kuvamiwa akiwa nyumbani kwake.


Taarifa za awali zinasema kuwa usiku huu umeme ulikatika katika nyumba yake. Luena akatoka nje kutizama kama kuna shot maana nyumba za jirani zilikuwa na umeme. Alipozunguka nyuma ya nyumba yake kukagua umeme akakutana na kikosi cha watu wenye mapanga wakamkatakata hadi wakamtoa roho.
Share To:

msumbanews

Post A Comment: