Wananchi Jijini Arusha wamemuomba waziri wa maji Jumaa Aweso kuingilia kati mikataba ya Wakandarasi wanaopewa mikataba na Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Arusha (AUWSA ) kama kunakipengere cha kurekebisha barabara baada ya kupitisha miradi ya mambomba ya Maji taka katika barabara za mitaa wafanye hivyo maana wamekuwa wakichimba barabara hizo bila kuzirudishia katika hali yake ya awali kama zilivyokuwa awali kabla ya Mabomba kupita .Wananchi wanaotumia barabara ya Bar Mpya kushuka Transformer kuelekea Msasani B kwa Murombo jijini Arusha wamekuwa ni wahanga wa kadhia hiyo barabara ilitengenezwa vizuri kwa pesa za serikali mwezi wa 8 mwaka jana mwezi wa 10 wakachimba barabara hiyo na kuiacha hivyo hivyo hadi leo hii kwa takribani miezi Saba huku wakiweka chemba za mifuniko katikati ya barabara zikiwa zimetokeza you hali inayosababisha kero kubwa kwa vyombo vya Moto kwa watumiaji wa Barabra hiyo.


Wananchi wa eneo hilo walieleza kuwa walishafikisha kilio Chao TARURA wakaambiwa wenye jukumu la kurekebisha barabara hizo ni AUWASA na walipoenda AUWASA wakajibuwa kuwa Mkandarasi atarekebisha lakini haikuwa hivyo.


Share To:

Post A Comment: