Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, ameipa Serikali siku tano kutoa kauli Bungeni kuhusu hatua za dharura ambazo inazichukua ili kudhibiti ongezeko la bei ya mafuta nchini hali iliyosababisha kupanda kwa gharama za maisha.


Agizo hilo limetolewa leo Mei 5, 2022 Bungeni Jijini Dodoma baada ya hoja ya dharura iliyotolewa na Mbunge wa Kilindi, Mhe. Omary Kigua ya kuliomba Bunge lijadili na kutafuta suluhu ya kuwapunguzia Wananchi ukali wa maisha unaosababishwa na ongezeko la bei ya mafuta.

Share To:

Post A Comment: