Na Elizabeth Joseph,Monduli.


Halmashauri ya Wilaya Monduli imejivunia kuvuka malengo ya Uandikishaji wa Anwani za Makazi kwa asilimia 101.


Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Raphael Siumbu wakati akiongea na chombo hiki kuhusu utekezalaji wa zoezi hilo.


Siumbu alieleza kuwa katika zoezi hilo hadi sasa nyumba zote zimeshawepewa namba za utambuzi huku zoezi la kutengeneza vibao vya kuandika majina ya mitaa na barabara likiendelea.


"Zoezi la kuandika vibao limechelewa kutokana na kutokuwa na fedha hivyo Halmashauri tumejikusanya tayari fedha zimepatikana na kazi ya kutengeneza vibao inaendelea  tutaimaliza kwa wakati kabisa mitaa na barabara zetu zitatambulika vizuri"alifafanua Mkurugenzi huyo.


Aidha alitaja baadhi changamoto zilizojitokeza katika zoezi la Uandikishaji wa Anwani hizo kuwa ni pamoja na tatizo la wananchi kutojua mipaka ya maeneo yao pamoja na baadhi ya watendaji kutokuwa makini katika kuhakikisha nyumba zote zinapewa namba hivyo kusababisha baadhi ya nyumba kutopata namba Jambo alilosema tayari wamelishughulikia.


Zoezi la Anwani za makazi nchini linaendelea nchini kote ambapo linatarajiwa kukamilishwa Mei 2022.

Share To:

Post A Comment: