Meneja mahusiano Itel Tanzania bw. Fernando Wolle akimkabidhi baadhi ya vitabu Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ubungo NHC, Paul Mdachi katika hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika shule ya msingi Ubungo NHC leo 29 April 2022 jijini Dar es salaam.
Meneja mahusiano Itel Tanzania bw. Fernando Wolle akifafanua jambo katika hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika shule ya msingi Ubungo NHC leo 29 April 2022 jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Kampuni ya simu ya Itel Mobile Limited imetoa msaada wa Vitabu vya kiada vya masomo ya Sayansi, Hisabati na kingereza, shelfu 20 za kutunzia vitabu kwa watoto wanaotoka katika mazingira magumu wanaosoma katika shule ya Msingi Ubungo NHC.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada huo jijini Dar es salaam, Meneja mahusiano Itel Tanzania bw. Fernando Wolle amesema lengo la kutoa msaada huo wenye thamani ya shilongi million 5 ni kuunga mkono jitihada za serikali kuhakikisha kunakuwepo na mazingira mazuri ya kusomea na vitendea kazi mashuleni.

"Hakuna asiyefahu kuwa watoto ni hazina na ni taifa la lijalo, Itel kupitia kupitia kauli mbiu yetu ya "Enjoy Better Life" tumekuwa tukisaidia wanafunzi/ watoto jasa wanatoka katika mazingira magumu kuwa na mazingira mazuri ya kujisomea au vitendea kazi mashuleni" Alisema Bw.Wolle.

Alisema kupitia program hiyo, Itel Tanzania imekuwa wakitoa misaada ambayo itasaidia kutengeneza mazingira bora lengo la kuwasaidia watoto kufurahia maisha bora pamoja na mazingira bora ya kusomea. 

"Kupitia program yetu ya CSR ambayo imeanzishwa mwaka 2003 imekuwa ikirudisha fadhila kwa jamii na imekuwa ikitekelezwa katika nchi zote za afrika ambazo Itel inapatikana" Alisema Bw. Wolle.

Bw Wolle aliongeza kuwa kupitia program hiyo Itel Tanzania tayali wameanzisha mradi wa maktaba unaojulikana kama "wandering libraries project" ambao utachangia maktaba ndogo zaidi ya 10,000 kote barani afrika katika kipindi cha miaka 3. 
Meneja mahusiano Itel Tanzania bw. Fernando Wolle akikabidhi vifaa mbalimbali kwa wanafunzi wa shule ya msingi Ubungo NHC, kulia kwake ni Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ubungo NHC, Paul Mdachi katika hafla iliyofanyika leo 29 April 2022 jijini Dar es salaam



Share To:

Adery Masta

Post A Comment: