Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.


Katika kipindi cha Mwezi Julai,2021 hadi Machi,2022 halmashauri zote nchini zimefanikiwa kukusanya jumla ya Tsh. Bilioni 675.8 sawa na asilimia 78% ya makisio ya mwaka.


Hayo yamesemwa leo Mei,5,2022 jijini Dodoma na Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais,Tawala za mikoa na serikali za Mitaa [TAMISEMI Innocent Bashungwa wakati akiwasilisha taarifa ya ukusanyaji mapato ya ndani kwa halmashauri kwa kipindi cha Julai 2022 hadi Machi,2022 ambapo kwa mwaka wa fedha 2021/22 halmashauri zimepanga kukusanya Tsh.Bilioni 863.9.


Waziri Bashungwa ametaja halmashauri zilizoongeza jitihada za ukusanyaji mapato kuwa ni halmashauri ya Ngorongoro kwa asimilia 34%,Mtama 36%,Kishapu 36%,Bariadi 36Lindi  36%  ambapo hapo nyuma zilikuwa za mwisho huku halmashauri zilizoshuka ukusanyaji mapato kuwa ni pamoja na halmashauri ya Msalala ikishuka kwa asilimia 38% kutoka asilimia 117%.


Katika hatua nyingine,Waziri Bashungwa amewabadilishia vituo   wakuu wa vitengo vya fedha 109  huku wengine 16 wakibadilishiwa majukumu.


Halmashauri  5 zilizofanya vizuri  ukusanyaji mapato ni pamoja na halmashauri ya Mbulu  TC 89.63%,Babati  DC 89.53%,Mtwara DC  88.67%,Ludewa  DC88.30% na Songea DC kwa 86.68 huku halmashauri 5 zilizofanya vibaya  ni pamoja na halmashauri ya Kigoma  45.49%,Serengeti 45.19 %,Bumbuli 43.55%,Nkasi  41.26%, na Bunda 37.53% .


Halikadhalika kwa mwaka huu uchambuzi wa makusanyo  umeongezwa kwa vigezo 6 ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya ndani,ujibuji wa hoja za ukaguzi za CAG,matumizi ya mapato ya ndani katika miradi ya maendeleo,utoaji wa mikopo kwa vikundi ya 10% ya mapato ya ndani,usimamizi wa urejeshaji ya mikopo ya vikundi na kigezo cha sita ni matumizi ya fedha za marejesho.


MWISHO.

Share To:

JUSLINE

Post A Comment: