Kwanz kabisa bangi ni neno ambalo hutumika kuelelezea sehemu iliyokaushwa ya maua, mbegu, mche na majani ya mmea ujulikanao kama Indian hemp. Mmea huu huko mitaani una majina mengi, majina hayo ni kama: dope, nyasi, majani, mche, ganja, magugu, kitu, sigara kali, blanti na mboga.

Kwa kitaalam “cannabis” huelezea aina mbali mbali za dawa za kulevya zitokanazo na mmea wa Indian hemp ambazo ni bangi (marijuana) na hashish.

Aina hizi za dawa zitokanazo na mmea huu ziko katika kundi la dawa za kulevya ziletazo maruweruwe (hallucinogen) au dawa zinazoathiri ubongo na kubadili jinsi tunavyotazama mambo katika uhalisia wake, nan do maana mtu akitumia bangi mara nyingi hufanya vitui vya ajabu sana.

Kuna zaidi ya aina 400 za kemikali katika mmea huu na kemikali ya kulaumiwa inayohusika na mabadiliko haya katika ubongo hujulikana kama tetrahydrocannabinol (THC). Kiasi cha THC hutofautiana kulingana na eneo ulikolimwa mmea wa Indian hemp.

Kama tulivyoona bangi ni sehemu iliyokaushwa ya majani, mbegu, maua, na mche na huwa na rangi ya kijani, kijivu au brauni, lakini bangi ni dawa ya kulevya ambayo hutumika kinyume cha sheria katika sehemu nyingi duniani.

Bangi hutumika kwa kuvuta moshi kutoka katika msokoto, sigara iliyoungwa au bomba maalum ya kuvutia moshi wake. Wakati mwingine watumiaji hupukutisha sigara na kujaza bomba la sigara bangi au bangi iliyochanganywa na dawa nyingine za kulevya kama cocaine na aina hii hujulikana na watumiaji kama “blunt”

Mtumiaji anapovuta msokoto wa bangi, huanza kufanya kazi baada ya dakika chache na mvutaji huanza kuhisi mapigo ya moyo yakienda mbio, mapokeo ya uhalisia huanza kubadilika na kuona vitu visivyo katika uhalisia (ndoto za  mchana/ maruweruwe). Matokeo haya ya muda mfupi baada kuvuta moshi wa bangi, huweza kudumu kwa muda wa saa mbili hadi nne au kuendelea kwa muda mrefu zaidi ikitegemea na kiasi cha THC kilichovutwa na ukali wake.

Mara nyingi wavutaji wa bangi huvuta moshi kwa nguvu ndani ya mapafu na kuushikilia kwa muda mrefu ili kuongeza ufanyaji kazi wa THC ukilinganisha na anayevuta sigara na hii husababisha madhara makubwa katika mapafu ya mvutaji. Mbali na maudhi kama kukohoa na koo kuwasha, imeonekana kuwa uvutaji wa aina hii wa moshi unamweka mvutaji katika hatari mara tano zaidi ya kupata saratani ukilinganisha na mvutaji sigara.

Matatizo ya ubongo yanayopelekea kuathiri afya ya akili ni ugonjwa mbaya uwapatao wavutaji wa bangi. Anayevuta bangi huwa na uwezo mdogo wa kumbukumbu na pia humuondolea uwezo wa asili wa kufanya maamuzi yaliyo sahihi ukilinganisha na mtu asiyevuta bangi.

 Hivyo kila wakati kwa ulinzi na usalama wa afya epuka matumizi ya bangi.
Share To:

Post A Comment: