Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Basila Mwanukuzi (kulia) akimkabidhi cheti Shukrani Dickson (kushoto)  ambaye amemuwakilishi Meneja wa Shirika la World Vision Tanzania (WVT) Kanda ya Mashariki Juliana Charles kwenye Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda. Cheti hicho ni kutambua mchango wa shirika hilo katika kuisaidia jamii kwenye shughuli za ujasiriamali na huduma za jamii. (Picha na Yusuph Mussa). 

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Basila Mwanukuzi (kulia) akitoa cheti kwa mmoja wa wanawake wajasiriamali ambao walishiriki maonesho ya bidhaa za  wajasiriamali wanawake ambao baadhi yao waliwezeshwa na Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki, na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, na maonesho hayo yalifanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani  katika Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda. (Picha na Yusuph Mussa). 

Mwakilishi wa Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki  Shukrani Dickson, akisoma taarifa ya shirika hilo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Basila Mwanukuzi. Ni  kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda wilayani Korogwe. (Picha na Yusuph Mussa). 

Mkuu wa Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Basila Mwanukuzi (kushoto) akikagua mabanda ya bidhaa za  wajasiriamali wanawake ambao baadhi yao waliwezeshwa na Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki, na Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe, kwenye maonesho yaliyofanyika katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika kiwilaya katika Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda. (Picha na Yusuph Mussa). 

Watumishi wa Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki lenye Makao Makuu yake Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakipiga picha ya pamoja nje ya ofisi hiyo wakiwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki Juliana Charles (katikati), kabla ya kuelekea Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yanafanyika Machi 8 kila mwaka duniani kote. 

Watumishi wa Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki lenye Makao Makuu yake Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakipiga picha ya pamoja nje ya ofisi hiyo kabla ya kuelekea Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yanafanyika Machi 8 kila mwaka duniani kote. 
Watumishi wa Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki lenye Makao Makuu yake Wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wakipiga picha ya pamoja nje ya ofisi hiyo wakiwa na Meneja wa Kanda ya Mashariki Juliana Charles (kulia), kabla ya kuelekea Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda katika Halmashauri ya Wilaya ya Korogwe kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo yanafanyika Machi 8 kila mwaka duniani kote. 


Na Yusuph Mussa, Korogwe

KATIKA kuhakikisha Taifa na jamii kwa ujumla inakuwa na "Kizazi cha usawa na haki kwa maendeleo endelevu", Shirika la World Vision Tanzania (WVT) limeendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kutekeleza shughuli mbalimbali zenye lengo la kukuza usawa wa kijinsia na kupinga  kila aina ya ukatili na uonevu dhidi ya mwanamke na mtoto wa kike kwenye jamii.

Moja ya njia ya kukuza usawa huo wa kijinsia ni kuboresha mazingira ya kusomea na kujifunzia, ikiwa ni pamoja na kuongeza vyumba vya madarasa na madawati pamoja na kununua vitabu kwa ajili ya shule za umma ili kuhakikisha watoto wa jinsia zote wanapata fursa ya kuendelezwa.

Hayo yalisemwa Machi 8, 2022 na Meneja wa Shirika la World Vision Kanda ya Mashariki  Juliana Charles  kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yaliyofanyika Kijiji cha Gereza East, Kata ya Kwagunda wilayani Korogwe.

Akisoma taarifa ya shirika hilo kwa niaba ya Meneja wa Shirika hilo,  mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi ambaye ndiyo alikuwa mgeni rasmi, Shukrani Dickson ambaye ni Meneja Mradi wa Sauti Vijana, Mnyuzi AP na Mkumburu AP, alivitaja vipaumbele vingine katika kumkomboa mtoto wa kike.

"Kuendesha kampeni za kupinga  na mimba za utotoni, kupinga mila potofu ikiwemo ukatili dhidi ya mwanamke kupitia mafunzo ya kufurahia familia na mtazamo chanya ambayo yanatekelezwa sambamba na programu zingine za maendeleo katika jamii, 

"Kutekeleza miradi ya maji inayolenga kuongeza upatikanaji wa maji karibu na kaya ili kumpunguzia mwanamke adha ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji, badala yake atumie  muda huo kuhudumia familia na kufanya shughuli za uzalishaji mali, na kuwezesha upatikanaji wa elimu ya ujasiriamali kwa makundi mbalimbali na kujikwamua kiuchumi" alisema Meneja

Shughuli nyingine katika mapambano hayo, ni kuwezesha upatikanaji wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati kwa lengo la kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, na kuboresha miundombinu ya zahanati au vituo vya afya  kwa kujenga majengo ya mama na mtoto, au majengo ya huduma za wagonjwa wa nje (OPD) kulingana na mahitaji.

"Kuboresha miundombinu ya usafi ikiwemo vyoo kwenye taasisi za elimu ili kumsitiri mtoto, hususani wa kike kusudi aweze kupata elimu ya msingi ama sekondari katika mazingira rafiki. Jitihada hizi kwa namna moja ama nyingine, humgusa mwanamke na mtoto wa kike na kumuongezea fursa za maendeleo ambayo ni endelevu" alisema.

Meneja Charles alipendekeza njia muhimu za kujenga usawa wa kijinsia na uendelevu katika Taifa na jamii kwa ujumla kuwa ni kuongeza uwakilishi wa wanawake katika uongozi na nafasi za maamuzi, ambapo katika Siku ya Wanawake Duniani, Shirika la World Vision linaungana na asasi nyingine za kiraia kutoa wito wa mageuzi ya kisera na kijamii ambayo yataweka usawa  wa kijinsia na uendelevu katika maendeleo.

Meneja alisema pia kuwawezesha wanawake kuwa wazalishaji wadogo. Katika miongo michache iliyopita, asilimia 55 ya uboreshaji  uliofanywa katika nyanja ya usalama wa chakula katika nchi zinazoendelea, umechochewa na programu zinazoshughulikia uwezeshaji wa wanawake. 

"Utafiti uliofanywa na Shirika la Chakula na Kilimo Duniani (FAO), unaonesha kuwa kama wakulima wanawake wangekuwa na uwezo wa kupata rasilimali za uzalishaji kama walionao wanaume, uzalishaji ungeongezeka kwa asilimia 20 hadi 30 kuliko ilivyo sasa, hivyo kupunguza njaa duniani kwa asilimia 12 hadi 17 kuliko ilivyo sasa" alisema Meneja.

Mkuu wa Wilaya, Mwanukuzi, alisema mwanamke ni mtu muaminifu kwenye maisha yake ya kila siku, iwe kwenye kazi za kuajiriwa ama kujiajiri, kwani yupo tayari kupambana kuona familia yake inapata mahitaji muhimu kwa namna yeyote ile. Ametaka wanawake wapate elimu, kuwajengea uwezo na kujitambua.

Mwanukuzi ametaka halmashauri na asasi nyingine kutoa  mikopo kwa wanawake ili kuweza kufanya ujasiriamali, huku akiwapongeza Shirika la World kwa kuwawezesha wanawake kwenye shughuli za ujasiriamali kwa kuviwezesha vikundi na kuweza kutengeneza bidhaa mbalimbali. 

MWISHO.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: