Na Prisca Libaga Maelezo Arusha Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela amewataka watanzania kuungana na wanawake katika maadhimisho ya wiki ya siku ya wanawake duniani ambapo mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho hayo atakuwa waziri Gwajima. Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha Mongela amesema kuwa usawa wa kijinsia unapaswa kupewa kipaumbele na ushiriki wa wanawake katika maadhimisho hayo yatakayoenda sambamba na matukio kadhaa hadi kilele. Alisema kwamba kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya wiki ya siku ya wanawake duniani "Haki usawa kwa maendeleo endelevu tujitikeze kuhesabiwa" Alisema kuwa tarehe nne wanawake watatembelea wodi za kinamama katika hospitali ya Mount Meru na kufanya usafi kutoa misaada ya vifaa katika wodi za kinamama. Mongela Pia alibainisha kwamba tarehe 5 wanawake watapata fursa ya kutembelea hifadhi ya Ngorongoro na Mgeni Rasmi atakuwa Mary Masanja Naibu waziri Maliasili na Utalii sanajari na mbio za kilometa tano na kumi kwa wanawake. Kwa Upande wake Afisa Maendeleo ya jamii mkoa wa Arusha Blandina Nkini alifafanua kuwa mbio hizo mgeni Rasmi atakuwa Pauline Gekul sanjari na Kongamano la wanawake litakaloendeshwa na chuo cha maendeleo ya jamii Tengeru. Akifafanua zaidi alisema kwamba siku ya tarehe 7 kutakuwa na maonesho ya watoa huduma za wanawake itakayoenda sambamba na siku ya kilele uzinduzi wa kanzi data ya wanawake na uongozi Tanzania Alieleza Nkini kwamba Mgeni rasmi wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani atakuwa Waziri wa maendeleo ya jamii jinsia wanawake na makundi Maalumu Doroth Gwajima.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: