Mwakilishi wa Balozi wa Uswiss nchini Tanzania, Leonor Bottaro akizungumza kuhusu maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Francophonie.
Balozi wa Morocco nchini, Zacharia El Goumiri akizungumza kuhusu siku ya kimataifa ya Francophonie.
Msaidizi wa balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Profesa Jean Kitembo, Nadhege Bini Kitenga ambaye naye alikuwa miongoni mwa wadai walioshiriki kwenye mkutano kuzungumzia wiki ya sherehe za wanachama wanaozungunza lugha ya Kifaransa.
Balozi wa Ufaransa nchini Nabii Hajloui akizungumza mbele ya waandishi wa habari( hawapo pichani) kuhusu sherehe ya wiki ya wanachama wanaozungumza lugha ya Kifaransa .Mkutano huo umefanyika kwenye kituo cha utamaduni cha ubalozi huo Allience Franciese  jijini Dar es Salaam.


 WADAU wa nchi wanachama ambao wanazungumza lugha ya Kifaransa wakiwemo mabalozi wa nchi 13 zinazoongea lugha hiyo wamekutana katika Kituo cha Utamaduni cha Alliance Francies kinachomilikiwa na ubalozi wa Ufaransa nchini Tanzania kwa ajili ya uzinduzi wa kusherehekea Wiki ya lugha ya Kifaransa 'francophonie.


Akizungumza leo Machi 7,2022 kwenye kituo hicho Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Nabil Hajloui amewaambia wawakilishi wa nchi ambazo zinazoongea lugha ya Kifaransa walioko nchini Tanzania wakiwemo mabalozi 13 ambao ni wanachama wa jumuiya ya Kimataifa ya Francophonie(OIF)kwamba wanasherehekea lugha ya Kifaransa kwa lengo la kukuza lugha hiyo inayozungumzwa na mamilioni ya watu Duniani kote.

Balozi Hajloui amesema katika kusherehekea wiki hiyo ya uzungumzaji Kifaransa kutakuwa na matukio mbalimbali yanayoendelea katika Ubalozi wa Ufaransa nchini kupitia kituo hicho cha Utamaduni na kwamba hakutakuwa na malipo kwa watakaohudhuria matukio hayo kuanzia Machi 9 Hadi Machi 26 mwaka huu.

Ametumia nafasi hiyo kutaja baadhi ya nchi aambazo ni nchi wanachama wanazungumza lugha ya Kifaransa ni Ubeligiji,Burundi,Canada,Congo,Comoro,Misri,Ufaransa ,Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Morocco, Rwanda, Senegal, Seychelles, Uswisi,na Vietnam ambao hao wote ni wanachama wa Jumuiya ya kimataifa ya Francophonie.

Akielezea zaidi kuhusu mtukio yatakayofanyika katika kusherehekea lugha ya Kifaransa, kutakuwepo na Tamasha la Walewale, kundi franco -Tanzania litakalotumbuiza katika jukwaa la Allience Francaise Dar es Salaam Machi 9.Pia Onesho la filamu ya Tapis Rounge''(red Capet'') iliyopendekezwa na ubalozi wa Uswisi ambayo itaononyeshwa kwenye Kituo hicho Machi 11 jioni.

Matukio mengine ni maonyesho ya sanaa na Tamasha, Tamasha la fariji, bendi ya Kikongo pamoja na Makadirio ya filamu ya Canada iliyopendekezwa na ubalozi wa Canada na kuoneshwa na Allience Francaisee Dar es Salaam.

Kwa upande wao Wawakilishi wa jumuiya ya wanachama wanaozungumza lugha hiyo wakiwemo mabalozi wa nchi zinazoonheau Kifaransa waliopo nchini wakitoa historia fupi ya kusherehekea lugha hiyo wamesema waanzilishi wa Shirika la kimataifa la Drancophonie ( OIF) walikuwa Leoppold S. Senghor ambaye ni Rais wa zamani w Senegal, Habib Bourguib na Hamani Diori wenzake wa Tunisia na Nigeria pamoja Prince Norodom Sihanouk wa Cambodia.

Wamesema lengo lao lilikuwa kutumia lugha ya Kifaransa kama njia ya kukuza mshikamano na maendeleo, na kuleta jumuiya mbalimbali pamoja. Maono yao yalitimia ilipofika machi 20, mwaka 1970 huko Niamey (Niger) ambapo mataifa 21 na serikali zilitia saini mkataba wa kuunda wakala wa ushirikiano wa kitamaduni na kiufundi (ACCT).

Wawakilishi hao wamefafanua Kifaransa kilikuwa kitovu cha shirika kwa lengo la kupanua mawasiliano ya kiutamaduni na kiufundi kwa wanachama na mwaka 1998 ACCT ikawa shirika la kiserikali la francophonie na tangu mwaka 2005 imekuwa ikijulikana kama OIF na tarehe ya kuundwa kwa ACCT Machi 20 ilichaguliwa mwaka 1998 kuadhimisha siku ya kimataifa ya francophonie OIF.

Wamesema OIF ni chombo chenye nguvu cha ushirikiano na kubadilishana kitamaduni kati ya wanachama wake, haswa kwa kukuza lugha ya Kifaransa na anuai ya lugha na kitamaduni,pia kwa kushirikiana katika nyanja zingine kama vile amani, demokrasia na haki za binadamu na msaada kwa kielimu, mafunzo,elimu ya juu na utafiti. Hivyo leo OIF inajumuisha nchi 54 wanachama.

Kuhusu lugha ya Kifaransa wadau hao wamesema lugha hiyo ni ya tano inayozungumzwa zaidi duniani na kwa Sasa Kuna wazungumzaji zaidi ya milioni 300 duniani kote na kufikia mwaka 2070 idadi ya wazungumzaji wa lugha ya Kifaransa inatarajiwa kuongezeka hadi milioni 800.

Kwa mujibu wa Wawakilishi wa nchi zinazoongea Kifaransa wamesema ni lugha rahisi katika nchi 32 na katika mikoa na idara zote za Ufaransa za anga,ambo inatumiwa katika mashirika mengi ya kimataifa pamoja na umoja wa Afrika.

Pia wamesema Kifaransa inachukuliwa kuwa lugha ya kimataifa ya kidiplomasi na inabakia kuwa lugha ya pili ya kidiplomasia kwa taasisi nyingi za kimataifa.Ni lugha ya kufundisha kwa zaidi ya watu milioni 132 na lugha ya nne inayotumiwa kwenye mtandao.

Aidha ni lugha ya pili ya kimataifa inayotumiwa zaidi katika vyombo vya habari na muhimu zaidi, ni lugha ya tatu muhimu ya biashara na watanzania ni zaidi ya watu milioni 1.5 wanazungumza Kifaransa hasa maeneo ya Kigoma.

Kuhusu Tanzania wadau hao wamesema idadi inayoongezeka ya wanafunzi na wataalamu wanajifunza Kifaransa .Nia hiyo ya lugha ya Kifaransa inaweza tu kusifiwa katika nchi ambayo ina majirani kadhaa wanaozungumza Kifaransa na ambayo imeonyesha dhamira yake kubwa ya kushiriki katika ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa wa Afrika.

Balozi wa Congo nchini Tanzania
Profesa Jean Kitembo amesema lugha ya Kifaransa ni kiunganishi kikubwa cha amani na utulivu duniani na kwa upande wa kwao Jamhuri ya Congo lugha hiyo inaanza kufundishwa kuanzia shule za awali hadi chuo kikuu. 

Share To:

Post A Comment: