Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar akizungumza wakati akifungua mafunzo  maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).
Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar akizungumza wakati akifungua mafunzo  maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT).

MMOJA wa wafanyabiashara walioshiriki mafunzo hayo akizungumza na waandishi wa habari ambapo alipongeza mfumo huo mpy

Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo
Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia mafunzo hayo



NA OSCAR ASSENGA, TANGA

 MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Tanga wametoa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini waliosajiliwa na kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kuhusu mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa Ritani ya Kodi la Ongezeko la Thamani (VAT).

Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo Afisa Elimu Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) Mkoa wa Tanga Salim Bakar wakati wa mafunzo maalumu kwa wafanyabiashara Jijini Tanga waliosajiliwa na kodi ya ongezeko la Thamani (VAT). 

Alisema mafunzo hayo yanakuwa endelevu kwa wilaya nyengine kuhusiana mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani za kodi la ongezeko la thamani (VAT) kwa walipa kodi pindi yanapojitokeza mabadiliko, marekebisho ya sheria za kodi lengo ni kukuza uelewa wa wafanyabiashara wanapotumia mifumo kuwasilisha ritanio za kodi.

 Alisema mamlaka hiyo imeanzisha mfumo wa uwasilishaji wa Ritani ulioboreshwa na ilitoa Taarifa mwezi February mwaka huu na kwamba kuanzia ritani za mwezi Machi za VAT ambazo zinawasilishwa mwezi Aprili walipa kodi watapaswa kutumia mfumo mpya ulioboreshwa wa uwasilishaji wa ritani.

 Afisa huyo alisema mfumo huo utakuwa na faida nyingi ikiwemo urahisi kwa mtumiaji ambapo mlipakodi atahitajika kutumia akaunti moja ya uwasilishaji wa ritani tofauti na awali ilikuwa ikimlazimu mlipakodi kutumia tofauti kulingana na aina ya ritani ya kodi.

 Aidha alisema faida nyengine ni ujazaji wa ritani umerahisishwa ambapo taarifa za manunuzu katika ritani ya VAT zitaingizwa kwa kutumia namba ya uthibitisho (Verfication Code) tu iliyopo katika risiti ya kieletroniki tofauti na awali ambapo itamlazimu mlipakodi kujaza taarifa za kadhaa kama Jina la Muuzaji, Namba ya Usajili wa VAT, Namba na tarehe risiti/ankra, Kiasi cha Manunuzi na VAT katika manunuzi husika.

 “Kwa kweli mfumo huo mpya utaongeza mapato ya serikali na lengo la serikali ni kumrahisishia mlipakodi atape huduma iliyoboreshwa bila kufika TRA na hivyo atapata kuwasilisha ritani akiwa ofisini au nyumbani bila kufika TRA”Alisema

Hata hivyo alisema mfumo huo utawezesha kufanyika kwa marekebisho ya kodi pale yanapotokea kama yalivyoanishwa katika sheria ya kodi la ongezeko la thamani sura ya 148 tofauti na utaratibu wa sasa ambapo mlipakodi alihitajika kuandika barua ya kutoa taarifa kwa Kamisha. 

Awali akizungumza mmoja wa wafanyabiashara hao kutoka SD Supermarket Moniraju Vasant alisema wanashukuru kupatiwa elimu hiyo ya mabadiliko hayo na kwamba mpango huo utakuwa ni mzuri kwa ajili ya kuboresha mapato TRA. 

Alisema pia utawapunguzia usumbufu wa kwenda TRA kupata huduma badala yake kutumia mifumo hiyo wakiwa ofisini kwao na hivyo kuwawezesha kutekeleza majukumu mengine

 

 

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: