Na Ahmed Mahmoud Utafiti ni moja ya eneo ambalo halijazungumzwa Sana katika mafanikio ya serikali ya awamu ya sita kipindi cha Mwaka moja madarakani wa Rais Samia Suluhu Hassan. Serikali imetoa fedha nyingi Sana ili nchi iendane na sayansi teknolojia na ubunifu chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) ambao ni kuwasadia wadau wa maendeleo chini yake taasisi na mashirika pia vyuo vya elimu ya juu na wabunifu katika kufanya Tafiti za Sayansi Teknolojia na Ubunifu. lengo ni kuongeza uelewa kutangaza maendeleo iliyopiga hatua serikali katika sayansi teknolojia na Ubunifu uliosimamiwa naTume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kipindi cha Mwaka moja wa Rais Samia Suluhu Hassan Sera za serikali na vipaumbele vyake mfano Kilimo Kwanza vimesaidiwa kufanya Utafiti katika maeneo ya Viwanda kilimo Afya na Ubunifu ili kukuza misingi mikubwa ya maendeleo ya Sayansi na teknolojia. Kwa kipindi kirefu Sasa watafiti wetu wameendelea kutoa tafiti kadhaa zenye kueleza na kubuni masuala mbalimbali kwa lengo la kuhakikisha nchi inapiga hatua kubwa kimaendeleo na kuendana na masoko ya kimataifa. KupitiaTume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ambao ndio wasimamizi wa wadau wa maendeleo wamekuja na mafunzo kwa waandishi wa habari na watafiti kuchakata habari za kiutafiti ambazo awali zilikuwa zikitolewa katika lugha ngumu ya kiutafiti ili walengwa ambao ni wananchi wanufaike na matokeo ya Tafiti. Baadhi ya taasisi wadau wa maendeleo waliochini ya COSTECH ni pamoja na Trido Temdo Camartec Tari na wabunifu Avomeru Imara na wengine wengi Hawa ni kwa uchache tu. Ni muda Sasa wa serikali ya awamu ya sita kuendelea kulitizama eneo hili na kulitengea fedha kuhakikisha mafanikio haya yanazidi kuipaisha nchi yetu kiuchumi kuendana maendeleo endelevu yalio katika sayansi na teknolojia. Fuatana na makala hii katika ziara ya siku mbili kutembelea watafiti mbalimbali na wabunifu wa mkoa wa Arusha iliyofanywa na wanahabari wa mikoa ya Arusha Manyara na Kilimanjaro. Baada ya semina ya siku nne iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ikiwa na lengo la kuandika Habari za kiutafiti sayansi teknolojia na Ubunifu kwa lugha rahisi ili kuwasaidia walengwa kunufaika na tafiti . Eneo hili la Utafiti limekuwa halipewi umuhimu mkubwa na vyombo vya Habari nchini kutokana na watafiti kuja na lugha za kiutafiti zaidi na mwisho wa siku Tafiti hizi kuandikwa kwenye majarida kwa lugha ngumu ambayo mlengwa hawezi kupata taarifa. Kuanzia Sasa wanahabari wataweza kuandika habari za sayansi ya Utafiti kwa kina baada ya mafunzo hayo ili mwananchi aweze kujua mbegu gani inafaa kwa msimu husika wa kilimo ili kuleta tija katika kukuza maendeleo ya sekta husika. Pia kujua sampuli za udongo wa eneo husika linafaa kwa mazao gani kuleta tija katika uzalishaji wa mazao bora na kusaidia kukuza pato la taifa Kuna msemo wa kiswahili unaosema"Mali bila daftari huisha bila Habari" kwetu kama taifa tunahitaji kubadilika kidogo kutoka kwenye kuandika tafiti na kuishia kwenye makaratasi na badala yake tafiti ziende kwenye jamii yetu. Tumeelezwa na kuona Watafiti wetu jitihada wanazofanya kuhakikisha tafiti zinapata matokeo chanya kwa jamii na kwenda mbele zaidi kuona nchi inapiga hatua za kimaendeleo. Ili kubadilisha uelewa wa wananchi kujua faida za tafiti katika biashara kilimo na hata uchimbaji wa Madini ambako jamii inapoteza fedha na nguvu nyingi bila mafanikio. Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia imeliona hilo na kuendelea kutoa fedha kwa taasisi na wadau wa maendeleo waliochini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na matunda tumeanza kuyaona ila waende mbali zaidi kutafiti katika upoteza matunda mfano Maparachichi Machungwa nk. Tunakapokuja na Tafiti ambazo hazifanyiwi kazi kwa muda muafaka hilo ni tatizo kubwa Sana katika maendeleo ya Sayansi na Teknolojia nchini hivyo busara za watoa maamuzi na watunga Sera kuangalia katika eneo hilo. Bila tafiti huna haki ya kueleza Jambo Sasa watafiti wetu wanafanya kazi kubwa ni kutafsiri tafiti hizo kuponya vidonda vya kukuza sekta za viwanda madini na kilimo katika kukuza pato la wananchi. Wizara ya kilimo imekuja na mkakati mkubwa wa kuongeza uchumi na pato la taifa tutumie tafiti zetu kutuongoza kufikia maendeleo ya Sayansi na teknolojia yatakayowasaidia wananchi kukuza vipato vyao kupitia kilimo. Tumeelezwa kwamba serikali imepima sampuli za udongo katika mikoa 14 kwa lengo la kuleta tija kwenye uzalishaji wa mazao nchini hili ni jambo muhimu Sana lililofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan. Kuna maeneo tulipatia na mengine tuliyakosea huu ni muda muafaka kuzipa tafiti zetu kipaumbele kwa maendeleo endelevu na sio kurudi nyuma katika kuacha tafiti zishindwe kuleta tija. Suala la fedha kwa watafiti liendelezwe ili kuyafikia maeneo mengi Sana mfano taasisi ya GST Biashara na kilimo kwa kuwalenga wachimbaji wadogo na wananchi wanaotafuta maeneo kwa mihemuko na Tafiti zisizo rasmi. Tujitahidi kutenga fedha za Bajeti kwa wabunifu wetu mfano mzuri ni Avomeru na Ubunifu wa Mafuta ya Parachichi bado wanachangamoto kadhaa zinazohitaji mkono wa serikali kufikia malengo ikiwemo vyumba vya baridi masoko ya mazao hayo ambayo yapo katika nchi za Asia lakini kutokana na usafiri wa mizigo inabidi mawakala wawepo nchi jirani ya Kenya. Tunahitajika kuyavuta masoko haya kuja nchini badala ya kuachia nchi nyingine kuwa madalali wa bidhaa zetu tunazozalisha hapa nchini kwa serikali kutoa fedha nyingi katika tafiti sayansi teknolojia na uzalishaji wa mbegu bora na ubunifu Kama tulivyosikia malengo ya serikali ya awamu ya sita ni kununua ndege ya mizigo huu Sasa ni wakati muafaka wa kununua usafiri huo kuwezesha mazao yetu yanasafirishwa moja kwa moja kuanzia hapa nchini kwenda Kokote duniani na pia kuyashawishi mashirika mengine kuleta ndege za mizigo.
Share To:

Arusha Newsroom

Post A Comment: