Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) Jerry Silaa  akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani.
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akizungumza wakati wa ziara ya kamati hiyo
Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  akizungumza wakati wa ziara hiyo kulia ni Mwenyekiti wa
Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo akisisitiza jambo wakati wa ziara ya kamati hiyo



NA OSCAR ASSENGA,MUHEZA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Uwekezaji na Mitaji ya Umma (PIC) imeishauri serikali kuangalia sheria ya usafirishaji wa viumbe hai nje ya nchi ilivyowaathiri wafugaji wa vipepeo wa Amani Wilaya ya Muheza mkoani Tanga

Kauli hiyo imetolewa na mwenyekiti wa kamati hiyo, Jerry Silaa wilayani Muheza wakati wa ziara ya kamati hiyo ilipotembelea Hifadhi ya Msitu wa Asili wa Amani.

Amesema Serikali ipitie sheria hiyo na kuangalia namna ambavyo wananchi waliokuwa wanafuga vipepeo na kuwauza nje nchi kwa ajili ya kujipatia kipato wameathirika.

"Serikali ilitoa katazo baada kuingia dosari ya kusafirisha viumbe wengine zaidi ya vipepeo, hivyo tunapendekeza ipitie sheria hiyo ili kuendeleza ufugaji wa vipepeo kwa wananchi na kujiongezea vipato vyao," amesema Silaa.
Pamoja na mambo mengine, kamati hiyo ilijionea miradi mbalimbali ndani ya hifadhi hiyo inayotekelezwa na TFS katika msitu huo.

"Tumejionea mambo mengi tukiwa katika hifadhi hii, aina mbalimbali za miti ambayo inapatikana hapa, ujenzi wa miundombinu ya barabara pamoja na njia za watembea kwa miguu na majengo na tumefurahishwa," amesema Silaa.

Aidha, amesema wajumbe wa kamati hiyo wameridhishwa na matumizi ya fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya maboresho ya miundombinu ya barabara na majengo.

Awali akizungumza wakati wa Kamati hiyo, Kamishna wa Uhifadhi wa Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) Profesa Dos Santos Silayo alisema maelekezo ya wizara watakwenda kufanyia kazi na suala la kusafirisha viumbe hai nje wameelekeza jambo hilo lifanyiwe mapitio kuona namna ambavyo suala la vipepeo vinaweza kufanyiwa utaratibu wa kisheria ili wananchi wa maeneo hayo waendelee kufaidika na utaratibu wa kufuga waone tija ya kushiriki kwao kwenye uhifadhi wa rasilimali za misitu kwenye eneo hilo.

“Tunahaidi kwamba tutakwenda kulifanyia kazi serikali yetu ni sikivu inaongozwa ya Rais wetu Samia Suluhu na tunaamini jambo hili litafanyiwa kazi na bunge wakati wote limekuwa likishauri kwenye masuala mbalimbali hivyo tunalichukua na katibu mkuu wetu atafikishiwa taarifa hizo kwa ajili ya utekelezaji”Alisema

Hata hivyo alisema wanaishukuru kamati kuwatembelea na kukagua miradi inayotekelezwa na serikali katika kufadhiliwa na fedha za kupunguza makali ya uviko 19 ambapo mradi umejengwa eneo la kuingilia eneo la hifadhi hiyo.

Alisema pia kuna mradi wa barabara ikiwemo wa kuboresha nyumba na makazi kwa ajili ya watafiti au watalii kwenye fedha za uviko ambapo msitu huo ulitengewa Sh.Million 502 kati ya shi Bilioni 4 ambazo TFS walipewa kutekeleza miradi kwenye msitu 11.

Naye kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Muheza Halima Bulembo  aliishukuru kamati hiyo kwa kuliona suala la vipepeo na walichobakia ni serikali kulifanyia utekelezaji vipepeo wilayani humo inaingia mapato kwa serikali ni shughuli ambazo ilikuwa inawasaidia kiuchumi pia wananchi.



Mwisho.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: