▪️Ataka pia upokeaji maoni ya uboreshwaji mitaala kukamilika


Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (Mb) amelitaka Baraza jipya la Taasisi ya Elimu Tanzania kuhakikisha zoezi la kukamilisha uandishi wa vitabu 69 vya kiada vya sekondari linakamilika kabla ya mwaka 2022 kuisha.


Ametoa kauli hiyo leo Januari 7, 2022 Jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Baraza la Saba la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ambapo amesema zoezi hilo limechukua takriban miaka mitano likiwa linasuasua na hivyo kuiletea lawama Serikali.


"Nataka kuona vitabu vyote vya sekondari vikiwa vimekamilika kabla ya mwaka 2022 kuisha. Wakurugenzi watakaoshindwa kusimamia zoezi hili muwachukulie hatua stahiki kwa kuwa wapo chini yenu," amesema Waziri Ndalichako.


Katika hatua nyingine Waziri Ndalichako ameeleza kutoridhishwa kwake na mwenendo wa upokeaji maoni ya uboreshwaji mitaala ambapo amesema mchakato huo umetumia muda mrefu na kutaka Baraza hilo kuhakikisha zoezi hilo linakamilika mara moja.


Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: