Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa leo Januari 20 , 2022 ametembelea Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) Kwa lengo la kujifunza  Shughuli mbalimbali za taasisi hiyo.


Dkt.Kiruswa alifika  Katika ofisi za GST na kusaini kitabu cha wageni na kuanza ziara ya kutembelea Kurugenzi za Taasisi Kwa lengo la kujifunza na kuangalia jinsi shughuli za Taasisi zinavyofanyika.


Sehemu alizotembelea ni pamoja na Makumbusho ya Miamba na Madini, Maabara ya Madini , Sehemu ya uzalishaji wa ramani za jiosayansi pamoja na eneo maalum la utunzaji wa taarifa za Taasisi ( Archives).


Baada ya ziara Katika maeneo hayo,  Mtendaji Mkuu wa GST Dkt. Mussa Budeba alitoa  wasilisho maalum kwa Naibu Waziri juu ya  historia ya GST pamoja na kazi mbalimbali zilifanywa na zile ambazo zinaendelea kutekelezwa  kupitia wataalam wake.


Baada ya kumalizika kwa wasilisho maalum , Naibu Waziri alipata fursa ya kukaa kikao  na Menejimenti nzima ya *GST* na kupongeza Kwa kazi nzuri zinazofanywa na GST Katika kuendeleza sekta ya Madini nchini.

Share To:

Post A Comment: