Na Rhoda Simba,Dodoma

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS)  imesema  katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2021 Julai hadi Septemba ,uchumi umeongezeka  hadi kufikia kiwango cha asilimia 5.2 kutoka asilimia 4.4 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Aidha, Pato la taifa  kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi shilingi trilioni 37.0 kutoka shilingi trilioni34.5 kipindi kama hicho mwaka 2020 ambapo pato halisi la Taifa  liliongezeka hadi Shilingi Trilioni32.0 mwaka 2021 kutoka shilingi trilioni30.3 katika kipindi kama hicho 2020.

Hayo yamesemwa leo Januari 4,2022 na  Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu za Uchumi kutoka NBS Daniel  Masolwa wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu  ukuaji wa uchumi kipindi cha Julai hadi Septemba 2021.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema katika kipindi cha robo tatu ya mwaka 2021 Julai hadi Septemba ,uchumi umeongezeka  hadi kufikia kiwango cha asilimia5.2 kutoka asilimia 4.4 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Aidha, Pato la taifa  kwa bei za miaka husika liliongezeka hadi sh trilioni 37.0 kutoka shilingi trilioni34.5 kipindi kama hicho mwaka 2020.

Vilevile, pato halisi la Taifa  liliongezeka hadi Shilingi Trilioni32.0 mwaka 2021 kutoka shilingi trilioni30.3 katika kipindi kama hicho 2020.

“Katika kipindi cha robo ya tatu ya mwaka 2021 pamoja na changamoto za UVIKO 19 uchumi umeendelea kuimarika ambapo shughuli za huduma ya malazi na chakula iliongoza kwa kiwango cha juu zaidi cha ukuaji wa asilimia 14.3,”amesema.

Kaimu Mkurugenzi huyo amesema ukuaji ulichangiwa na kuongezeka kwa watalii 243,565 walioingia nchini kipindi cha kuanzia Julai hadi Septemba 2021 ikilinganishwa na watalii 72,147 katika kipindi kama hicho mwaka 2020.

Hata hivyo makadirio ya ukuaji wa uchumi wa Dunia kwa mwaka 2021 kwa mujibu wa Shirika la fedha Dunia IMF  mwezi Oktoba 2021,uchumi wa Dunia kwa mwaka 2021 unatarajiwa kukua kwa kiwango cha asilimia5.9 kwa mwaka 2021 huku kwa mwaka 2022 yameendelea kubaki katika kiwango cha asilimia4.9 zilizokuwazimekadiriwa awali.

Amesema ukuaji wa uchumi katika Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kipindi cha Julai- Septemba 2021 umeendelea kuimarika kutoka kiwango hasi cha ukuaji hadi kiwango chanja.

Amesema kwa upande wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uchumi umekadiriwa kukua hadi asilimia 3.7 katika kipindi cha Julai- Septemba 2021

Kwa upande wa Nchi zilizo Kusini mwa Jangwa la Sahara,Kaimu Mkurugenzi huyo amesema makadirio ya ukuaji wa uchumi katika Nchi hizo yalionesha Oktoba 2021 kuongezeka kwa kiwango  cha ukuaji wa uchumi hadi asilimia 3.7 kwa mwaka 2021.

“Makadirio haya yanatarajia kuongezeka  kutokana na kuimarika  kwa usafirishaji wa bidhaa nje ambazo zimesaidia kukabiriana na madhara kuagiza zaidi bidhaa za chanjo ya UVIKO 19 kutoka Nje,”amesema.

 Mwisho.


 


Share To:

RHODA SIMBA

Post A Comment: