Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali sa Mitaa Mhe. Ummy Mwalimu amewasili Mkoani Tabora na kuanza ziara yake kwa kikao na Wataalam wa Sekretariet ya Mkoa huo sambamba na kupokea taarifa ya Mkpa iliyowasilishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dr. Batilda Buriani.


Amepongeza Mkoa huo kwa Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa kukusanya sh. Bil 13.8 sawa na asilimia 51 ya malengo waliyojiwekea ya kukusanya shilingi hil 26.9


Aidha amemuelekeza Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Dkt. Batilda Buriani kuzifuatilia kwa karibu Halmashauri ya Nzega Tc  na Nzega Dc kwa kuwa chini kimakusanyo; Nzega Tc wamekusanya asilimia 34%  na Nzega Dc wamekusanya asilimia 39 tu mpaka hivi sasa zikiwa chini ukilinganisha na  halmashauri zote za Mkoa wa Tabora.


Pia amewapongeza uongozi wa Mkoa wa kusimamia kikamifu utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kukamilisha ujenzi wa miradi ya maendeleo kwa ustawi husani madarasa.


Akizungumza katika kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mhe. Dkt. Batilda Buriani amesema katika ujenzi wa vyumba vya madarasa Halmashauri za  Tabora Manisapa na Nzega Tc wamekamilisha kwa asilimia 100 na halmashauri za Uyui, Urambo,Kaliua na Sikonge wakl kwenye asilimia 90 na kwa muda ulioongewa wa tarehe 31 Disemba,2021 watakua wamekamilisha kwa asilimia 100.

Share To:

Post A Comment: