KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema akizungumza wakati akifungua mkutano wa wadau wa NSFF katika mkoa wa Tanga uliofanyika leo

Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa NSSF Jijini Tanga leo

Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius akizungumza wakati wa mkutano wa wadau wa NSSF Jijini Tanga leo


AFISA Mwandamizi Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakar Mshangama Soud akizungumza wakati wa mkutano huo
AFISA Mwandamizi Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakar Mshangama Soud akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

AFISA Mwandamizi Mkuu wa NSSF Mkoa wa Tanga Abubakar Mshangama Soud akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo


Afisa kazi Mkoa wa Tanga Janeth Omolo akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo


Mansoor Ramadhani


Sehemu ya Washiriki kwenye mkutano huo
Sehemu ya washiriki kwenye Mkutano huo wakifuatilia matukio mbalimbali
Sehemu ya Washiriki wa mkutano huo



NA OSCAR ASSENGA, TANGA

KATIBU Tawala wa Mkoa wa Tanga Pili Manyema amewataka waajiri wenye malimbikizo wa michango katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSFF) kutumia fursa ya misamaha ya adhabu iliyotolewa na mfuko huo kuondoa malimbikizo waliokuwa wakidaiwa.

Pili aliyasema hayo leo wakati wa mkutano wa wadau wa NSFF katika mkoa wa Tanga ambapo alisema mkutano huu ni muhimu ambao dhumuni kubwa ni kutoa elimu juu ya shughuli za kiutendaji za mfuko NSSF, Sheria ya Hifadhi ya Jamii pamoja na kutatua changamoto zilizopo kwenye kufanikisha malengo ya kiutendaji mfuko na waajiri.

Alisema amefarijika sana uwepo wa mkutano huo kwani kufanya hivyo kutasaidia kuondoa yale malimbiko yaliyokuwa wanadaiwa huku akiwataka waajiri fursa hiyo muhimu kwa sababu kama walikuwa wanadaiwa tozo lakini kutokana na umuhimu wa kuwapunguzia.

Katibu Tawala huyo ambaye alimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema ni muhimu kuitumia ili kuweza kuona yale malimbikizo ya michango ya wanachama yanawasilishwa kwa wakati.

Alisema kwani michango hiyo mwisho wa siku inawasaidia wanachama wakati wanapokuwa wakistaafu kazi na inatia uchungu mwajiriwa anapostaafu anaanza kuhangaika na mafao yake kuwa sababu mwajiri hajawasilisha michango,

“Nitumie fursa hii mfuko wa NSSF kutoa punguzo kwenu kwa asilimia 75 ukipiga mahesabu utaona ni ela nyingi utakuwa umeiokoa hivyo utajipima mwenyewe kuona ..Lakini nafahamu zipo changamoto zinazowakabili waajiri kupitia changamoto hizo ni wajibu kuhakikisha michango inawasilishwa kwa wakati “Alisema

“Kwani michango hii itakwenda kuwasadia waajiriwa wanapostaafu hivyo naamini kupitia mafunzo hayo ambapo kwa sasa dunia imehama kutoka Analojia kwenda Digitali hivyo mtakapopata mafanzo hayo yatakwenda kuimarisha utendaji kazi kenye maofisi yao na kuondoka kwenye utendaji kazi wa mafaili na kwenda kutumia Tehama “Alisema

Hata hivyo aliwataka kutumia elimu waliyayapata kufikisha kwa wasaidizi wenu kwa sababu sisi ni binadamu tunaweze kupata changamoto kutokuwepo hivyo kukosekana kwenu kusikwamishe utendaji kazi katika ofisi zenu.

“Nikuombe Meneja wa Shirika la Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Tanga mafunzo hayo yawe endelevu kwa kuandaa mkutano kufanya tathimini kwa mfumo mlioanzisha ambao utakuwa na manufaa”Alisema

Hata hivyo Katibu Tawala huyo alisema mfuko huo umeanzisha huduma mbalimbali za kidigitali ili kurahisisha huduma kwa wadau wake huku akieleza Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga ina imani kwa ushirikishaji wa maoni ya wadau kwa sekta mbalimbali.

“Niwapongeze Ofisi ya NSFF Mkoa kwa mkutano huo kwani utaimarisha huduma za Hifadhi ya Jamii kwa mkoa na nchi kwa ujumla kwani Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu haipo nyuma kwenye kuongeza ustawi wa wananchi mmoja mmoja kwa sekta binafasi kwa ujumla”Alisema

Awali akizungumza wakati wa mafunzo hayo Meneja wa NSSF Mkoa wa Tanga Audrey Claudius alisema wamefanya mkutano na waajiri wasiopungua 900 na wamefanya kwa waajiri 120 wanashukuru mwitikio umekuwa mkubwa lengo likiwa ni kutoa elimu juu ya matumizi ya mfumo wa Tehama wanataka kuhama kutoka analogia kwenye kidigitali.

Alisema wameona watoe elimu kwa waajiri na zoezi hilo litakuwa endelevu ambapo wanataka kuona waajiri wote kuanzia mwezi Januari mwakani kutumia mifumo hiyo kufanya shughuli zao za kila siku au kuandikisha wanachama wapya kupata taarifa za wanachama.

“Lakini pia kulipa michango na wanapotumia mifumo hiyo wanajitahaidi kuhakikisha wanakuwa na data safi kwa sababu mifumo hiyo inawasaidia kupunguza data chafu na kupata taafisa sahihi za wanachama na wajiri wao,

Alisema wakishakuwa na taarifa sahihi watakuwa na data basee nzuri watakaohifadhi taarifa za wanachama wao na itawasaidia kutoa huduma bora baadae kwani mwanachama anapokuja kufuatilia mafao yake taarifa zake zitakuwa sahihi na hivyo kuweza kufanikisha.

Aidha alisema mwezi Octoiba Mosi mwaka huu wametoa taarifa kwamba watakuwa na punguzo za tozo kwa waajiri waliochelewa kulipa michango ya nyuma na tozo ilikuwa kwa awamu tano ambao hawajalipa michango kuanzia Octoba 1 hadi 31 walisamahewa tozo hizo asilimia 100.

Alisema sasa kwa awamu wa pili wamesahewa asilimia 75 ya tozo hivyo wanatumia mkutano huo kuwasihi waajiri wote watumie fursa hiyo kwani tozo hizo zitaisha Januari 31 mwakani watasamehe kwa asilimia 90 baada ya hapo haitakuwepo tena na taratibu wa kisheria zitafuata maana mchango wa NSSF ipo kwa mujibu wa sheria.

Kwa upande wake Afisa kazi Mkoa wa Tanga Janeth Omolo alisisitiza waajiri wanapo kuwa wakiajiri wanapaswa kuwa na mikataba ya kazi lengo kuu ni kuboresha mahusiano kati ya mfanyakazi na mwajiri.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: