Julieth Ngarabali, 


Serikali imekopesha watu wenye ulemavu sh. bilioni 12.9 hadi kufikia Agosti mwaka huu fedha zitokanazo na asilimia 10 za kwenye mapato ya ndani ya Halmashauri kote nchini.


Hayo yamesemwa mjini Kibaha Novemba 04 na Naibu Waziri ofisi ya Waziri mkuu Sera Bunge na watu wenye ulemavu Ummy Nderiananga kwenye maadhimisho ya siku ya Fimbo Nyeupe Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Pwani katika viwanja vya Mailimoja mjini Kibaha.


Naibu Waziri huyo amebainisha kuwa fedha hizo zimeweza kuwanufaisha watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wakiwemo wasioona nchini.

 

Amesema watu wenye ulemavu wana uwezo mkubwa kama walivyo watu wengine wasio na ulemavu  kwa sababu kundi hilo pia lina uwezo wa kufanya shughuli mbalimbali za kijamii na za kiuchumi.


Aidha Naibu Waziri huyo amewataka watu wenye ulemavu kitumia fursa ya sensa ya watu na makazi kujitokeza kwa wingi kuhesabiwa ili kupatikana takwiku sahihi ya kundi hilo.


 Naye Margareth Matonya mkurugenzi anayeshughulikia watu wenye mahitaji maalumu kutoka Wizara hiyo amesema mwaka 2021 wametoa mafunzo kwa walimu wapatao 1,373 kati yao  wathibiti ubora  ni 200 kwa lengo la kukagua na kuhakikisha miundombinu iliyopo na inayoendelea kujengwa ni rafiki.


Matonya ameongeza kuwa wathibiti ubora hao pia watafatilia kama inafikika eneo la ujifunzaji na ufundishaji na wanaangalia walimu wanavyofundisha wanafunzi wenye ulemavu lengo likiwa ni kuhakikisha kundi hilo linalata huduma sawa na wengine


Awali mwenyekiti wa Chama cha  Wasioona nchini (TLB)  Omary Sultan amesema maadhimisho hayo ni kwa ajili ya kukaa na kutafakari masuala mbalimbali ya wanachama ili kujua changamoto, mafanikio na kujifunza masuala mbalimbali yakiwemo ya kiuchumi, kijamii, afya na masuala ya maendeleo.


Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Kibaha Sara Msafiri ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Pwani amesema  mkoa huo umejenga mabweni kwa wanafunzi wenye mahitaji maalumu kwenye Halmashauri ya Chalinze na Mkuranga na kwamba mipango mingine zaidi ya kuboresha maeneo mengine yanafanyika.

Share To:

Post A Comment: