Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Hamad Chande akizungumza na Mabalozi wa Mazingira wakati akifungua warsha ambayo imewakutanisha mabalozi hao kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es salaam. Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Bi. Mary Maganga akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha mabalozi wa Mazingira kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es salaam. Mbalozi wa Mazingira wakifuatilia ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha Mabalozi wa Mazingira na kujadili kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.

Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Balozi wa Mazingira Alhad Mussa Salum akifuatilia ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha Mabalozi wa Mazingira na kujadili kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Mazingira ambaye pia ni msanii Mrisho Mpoto akifuatilia ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha Mabalozi wa Mazingira na kujadili kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam. Balozi wa Mazingira ambaye pia ni msanii Beka Flaver akifuatilia ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha Mabalozi wa Mazingira na kujadili kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.Balozi wa Mazingira ambaye pia ni msanii Monalisa akifuatilia ufunguzi wa warsha ambayo imewakutanisha Mabalozi wa Mazingira na kujadili kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es Salaam.Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Hamad Chande akipata picha ya pamoja na Mabalozi wa Mazingira wakati akifungua warsha ambayo imewakutanisha mabalozi hao kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili Jijini Dar es salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

***********************************

Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe.Hamad Chande amewataka mabalozi wa mazingira nchini kuhakikisha wanasaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira ili vizazi vijavyo viweze kukuta nchi ikiwa na mazingira mazuri.

Kauli hiyo ameitoa leo wakati akifungua warsha ambayo imewakutanisha mabalozi wa mazingira kuhusu utekelezaji wa kampeni kabambe ya Hifadhi na usafi wa mazingira inayofanyika kwa siku mbili jijini Dar es salaam.

Naibu Waziri Chande amesema kuwa serikali imewaamini na kuwapa ubalozi ili kusaidia jamii kuweza kuishi kwa amani bila ya taharuki inayosababishwa na uharibifu wa mazingira.

‘Niwapongeze sana wataalamu wetu kwa kuwatafuta watu wakawaweka mabalozi kwani bila kujisimamia wenyewe hatotoka mtu nje ya nchi aje asimamie mazingira yetu bali tunayasimamia wenyewe’amesema Naibu waziri Chande

Kwa upande wake Shekh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni Balozi wa Mazingira Alhad Mussa Salum amewakumbusha watanzania kuwa utunzaji wa mazingira ni jambo la ibada kwani kufanya uharibu ni hatari kwa binadamu na viumbe wote.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: