Thursday, 18 November 2021

MBUNGE ZUNGU AMPONGEZA NAIBU MEYA KIMJI KWA UWASILISHAJI ILANI

 


NA HERI SHAABAN


MBUNGE wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu amempongeza Naibu Meya wa  halmashauri ya Jiji la Dar salaam ambaye ni Diwani wa Kata ya Ilala , Saady Kimji ,kwa uwasilishaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.


Mbunge Zungu alitoa pongezi hizo Lamada Dar es Salaam leo wakati Naibu Meya Kimji akiwasilisha Ilani ya utekelezaji .


"Madiwani wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam hongereni mmechagua Naibu Meya mtekelezaji wa Ilani pia mfatiliaji nawaomba wakati ujao msifanye makosa mumchague Saady Kimji anatekeleza Ilani kwa vitendo" alisema Zungu.


Mbunge aliwataka  wananchi wa wilaya ya Ilala pamoja na Kata ya Ilala  washirikiane na Naibu Meya Kimji katika kutatua changamoto mbalimbali wakati wote.

,

Akizungumzia maendeleo ya Jimbo la Ilala alisema Barabara Kilometa 56 zitajengwa katika jimbo hilo mtandao huo wa barabara za ndani ukikamilika itakuwa ametatua changamoto ya miundombinu iliyopo jimbo la Ilala.


Akizungumzia sekta ya Afya iliyokuwa majengo ya Amana Social analifatilia eneo hilo halmashauri ya jiji kwa ajili ya mchakato wa kugeuza matumizi liwe kituo cha afya Ilala .


"Eneo la vijana Center Amana Social ni mali iliyokuwa halmashauri ya jiji iliyopita kwa sasa lipo chini ya halmashauri ya Dar es Salaam Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Ilala imeomba eneo hilo kwa ajili ya huduma za afya ,Amana ni Hospitali ya Rufaa ya mkoa hivyo wagonjwa wa Ilala watapatiwa huduma katika kituo cha afya hicho kikikamilika  " alisema Zungu.


Mbunge Zungu aliwataka Wananchi wa Jimbo la Ilala washirikiane pamoja katika kujenga Ilala


Akizugumzia bonde la Msimbazi wananchi wa Ilala ambao wanakumbwa na mafuriko Mto umepita upande wao alisema Serikali imeanza mchakato kwa ajili ya ukarabati mto huo na kuweka kingo kwa ajili ya kuzuia mafuriko.


Aliwataka wananchi wa Jimbo la Ilala kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Suluhu katika kuleta maendeleo na kukuza uchumi katika nchi yetu.Diwani wa Kata ya Ilala ambaye ni Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Saady Kimji alisema 

Kata ya Ilala amefanikiwa kujenga shule ya sekondari Mivinjeni madarasa manne shilingi milioni 80,000,0000/= zitatumika fedha mapato ya ndani kwa ajili ya kuondoa kero ya vyumba vya madarasa .


Diwani Kimji alisema pia shilingi miliomi 90,000,000/=  kutoka serikali kuu zimetumika kujenga mababara ya kemia,Biolojia na Fizikia katika sekondari hiyo .


Aidha alisema fedha zingine shilingi milioni 60, 000.000/= zimetumika kukarabati madarasa ya shule ya sekondari mivinjeni fedha zimetokana na mapato ya ndani ya halmashauri ya jiji mradi huo umeweza kuweka mazingira rafiki ya kujifunzia na kusoma.


Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  Kata ya Ilala Habib Nasser alipokea taarifa hiyo na kumpongeza Mh .Saady Kimji  kwa kuwasilisha taarifa nzuri kwa wakati.


Mwenyekiti Habib Nasser aliwakumbusha Wana CCM kukisemea chama cha Mapinduzi kila wakati kwa utekekezaji wa Ilani sambamba na kuwataka wanachama wa chama hicho kila wakati kuvaa sare katika mikutano yake.

No comments:

Post a Comment