Na Said Mwishehe,

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni mkoani Dar es Salaam Fatma Almas Nyangasa amesema mchakato wa kuwapanga wafanyabiashara kwenye rasmi yaliyotengwa kwa ajili ya biashara unakwenda vizuri na huduma zote muhimu zikiwemo za maji, umeme,choo na barabara vimeshawekwa, hivyo ni vema wote waliopewa maeneo wakaenda kufanyabishara zao.

Akizungumzia na waandishi wa habari baada ya kutembelea maeneo yote yaliyopangwa kwa ajili ya wafanyabiashara, Fatma Almas Nyangasa amesema maeneo ya kufanyabiashara yapo ya kutosha na baadhi ya wafanyabiashara wamejenga vibanda,wapo tayari kuanza biashara zao.

"Kwa kifupi Kigamboni maeneo yapo na kila mfanyabiashara amepewa eneo lake kwa ajili ya kufanyabishara na bado kuna nafasi katika maeneo mengine , hivyo wananchi ambao hawajapa maeneo waje tuwapatie,kikubwa tutajiridhisha tu kama kweli anafanyabiashara.

"Waandishi wenyewe mmejiridhisha baada ya kutembelea maeneo yaliyotengwa, yapo ya kutosha , wengine tayari wamejenga mabanda na wengine wametelekeza, kwa hiyo nachotaka kusema maeneo haya yapo tusitake kupotosha wananchi.Katika maeneo yaliyotengwa ilikiwemo hili la kwa Urasa umeme, maji na vyoo vya muda na vya kudumu vipo,"amesema Nyangasa.

Pia amesema waliopewa maeneo halafu wameyatelekeza ni vema wakaenda katika maeneo waliyopangiwa kwasababu katika hifadhi za barabara taratibu haziruhusu watu kufanyabiashara."Hivyo tutumie nafasi hii kutayatumia vema maeneo yaliyotengwa na halmashauri kwa ajili ya wafanyabiashara.

"Mwito wangu waliorejea barabarani wakumbuke kila mfanyabishara ndogondogo anatakiwa kupatiwa eneo rasmi la kufanyabiashara na hilo sisi kama Kigamboni tumetekeleza, kwa hiyo kama ulipewa eneo na umerudi kwenye yasiyo rasmi taratibu zikichukuliwa sio lawama ya halmashauri.

"Kwasababu tayari umeshapewa eneo , utakuwa wewe mwenyewe umeenda kutafuta eneo sio rasmi na wahusika wakikuchukulia hatua usitulaumu, kwa hiyo niwaombe maeneo haya tuliyopewa tuyatumie , itafika baada ya muda kama umepewa na hujakaa watapewa wengine.

"Na tukifika hatua hiyo tusilaumiane, haya ni masoko tumetengeneza na soko linahitaji wafanyabiashara wawepo na kama hawapo soko halitakwenda ndio maana tunasema wote walioko maeneo siyo rasmi waje maeneo rasmi.Watalaam wetu  wameeleza wanayoendelea kuyafanyika katika eneo la kuwekwa miundombinu,'amesema.

Amefafanua kwa hiyo hadhani kama kuna sababu nyingine ya wafanyabiashara waliopewa maeneo kutokwenda , ila kumekuwepo na propaganda."Watu wasisikileze maneno ya watu, ni wewe ni biashara yako, watu wamepewa maeneo na wametelekeza na ndio hao hao wanasema hawana maeneo.Niwasisitize tunaomba wote ambao wanafanyabiashara waje katika maeneo haya, huduma zote muhimu zipo".

Kwa upande wake Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) Wilaya ya Kigamboni Ramadhan Bilal amesema wao wameendelea kusambaza umeme katika maeeneo yote yaliyotengwa na halmashauri kwa ajili ya wafabiashara ndogondogo.

"Kwa hapa tuko Kwa Urasa na hapa kama mnavyoona soko limeanza kufanya kazi, na kama yalivyo maelekezo ya Mkuu wa Wilaya, TANESCO tumejipanga na tumehakikisha huduma ya umeme imepatikana kwenye eneo la soko na sasa tumeandaa mpango maalum wa kuwatambua wafanyabishara wote.

Wakati Meneja wa DAWASA Wilaya ya Kigamboni Tumain Mhondwa amesema kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya wameanisha maeneo yanayotakiwa kuwekwa miundombinu ya maji na kazi hiyo imeshaanza."Hadi kufikia Jumatatu wiki ijayo maeneo yote yaliyoanishwa yatakuwa na maji safi na salama kwa ajili ya matumizi".

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Soko la Kwa Urasa Athuman Makono amewahamasisha wafanyabiashara waliopewa maeneo hayo kwenda kuanza biashara zao kwani kwa sasa mwitikio umekuwa mdogo kwa waliopewa.

"Katika eneo wafanyabiashara kila mmoja analo  eneo lake, ni vema waje kufanya biashara, kama umepewa eneo halafu huji sasa ulilichukua kwa ajili ya nini?Kama hawataki waseme ili wapewe wengine wanaohitaji,'amesema.

Mmoja wafanyabiashara katika soko hilo Sheikh Baliz Abdallah ameishukuru halmashauri ya Wilaya ya Kigamboni kuwatengea maeneo ya kufanyabiashara likiwemo la Kwa Urasa. "Ombi letu eneo hili liendelee kuinuliwa ili wanaokataa hivi sasa waje waone wivu.




Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: