Na Rhoda Simba,Dodoma


BENKI ya Dunia imeridhishwa na maandalizi ya utekelezaji wa Mradi wa Tanzania  ya Kidijitali ambao utagharimu kiashi Cha Shilingi bilioni 349 zilizotolewa na Benki hiyo wenye lengo la kuboresha minara 488 toka uwezo wa 2G kwenda 4G2 na zaidi ya minara 300 itajengwa ili kuboresha huduma ya mawasiliano 

Akizungumza mbele ya ugeni toka Benki ya Dunia Nchini Marekani,Naibu Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Injinia Mathew Kundo amesema kuwa  Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miaka mitano   na utasaidia uboreshaji wa miundombinu ya TEHAMA ya Serikali,Miundombinu ya Taifa ya anwani za Makazi na posti Kodi,maendeleo ya Vijana na biashara ya mtandao.


" Mradi huu utaenda  kuboresha miundombinu ya tehama kwani miundombinu ya mawasiliano ni sawa na miundombinu ya barabara kama barabara ikiwa mbovu huwezi kufika haraka utafika kwa kuchelewa hivyo hata kwenye mawasiliano pia tunatakuwa kuwa na miundombinu bora na yenyekasi zaidi ," amesema Naibu waziri huyo.


Injinia Kundo Amebainisha kuwa Mradi huo una lenga kukuza maendeleo ya Kidijitali kama kichocheo Kikuu Cha ukuaji wa uchumi na ukuaji wa Viwanda,utengenezaji wa ajira,utoaji wa huduma na ufanisi wa Serikali.


Naye Katibu Mkuu wa Wizara hiyo,Dk. Zainabu Chaula amesema kuwa atahakikisha ansimamia Mradi huo kwa weledi mkubwa na kuzingatia uwazi kama Benki ya Duniania inavyotaka kwakuandaa mfumo wa utoaji maoni .


Kwa upande wake Justina Kajange akizungumza kwaniaba ya kiongozi wa msafara wa Benki ya Dunia amesema kuwa Mradi huo ulikuwa ni malengo ya muda mrefu toka Mwaka 2018 lakini wameridhishwa na maandalizi yake  hivyo Mradi utatekelezwa kama ulivyokusudiwa.

Share To:

Post A Comment: