JOSEFU Haule (25) mkazi wa kijiji cha Lupande kata ya mawengi wilaya ya Ludewa mkoani Njombe amehukumiwa kifungo cha miezi 11 jela jela au kulipa faini ya shilingi 300,000 baada ya kukiri kosa la kumtolea lugha ya matusi kwa maandishi mkuu wa polisi wilaya ya Ludewa SSP Deogratius Masawe.


Hukumu imetolewa jana Novemba 16 katika mahakama ya Mwanzo Mlangali wilayani humo na kudaiwa kuwa kosa hilo ni kinyume cha sharia namba 89vya mwaka 2019.

Imeelezwa kuwa mtuhumiwa huyo alifika hatua ya kuandika ujumbe wa matusi baada ya mama mkwe wake Berdeta Njelekela kutoa malalamiko ya kunyanyaswa kwa binti yake ambaye ni mke wa mtuhumiwa huyo katika mkutano wa hadhara uliofanyika 12/11/2021 ukiongozwa na mkuu wa polisi huyo pamoja na wawakilishi wa dawati la jinsia kutoka ofisi ya mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa Njombe.

Baada ya kutolewa malalamiko hayo ya unyanyasaji Masawe aliagiza Joseph Pamoja na mkewe Grace Lawrence kufika kituo cha polisi Mlangali ili waweze kusikilizwa migogoro yao ambapo katibu wa kitongoji Macarius Haule alifikisha barua ya wito lakini alijibiwa na mtuhumiwa kuwa hawezi kufika kufika kituoni hapo.

Hata hivyo mke wa mtuhumiwa Bi,Grace Lawrence alifika kituoni huku akiwa na barua ya wito waliyopelekewa ambayo chini yake iliongezewa maandishi yenye matusi na kusisitiza haendi kituoni hapo na OCD hamfanyi chochote.

Grace alieleza kuwa ujumbe huo umeandikwa na mume wake na kumkabidhi ili aifikishe kituoni huku akikiri kupata manyanyaso kutoka kwa mume wake ambapo jeshi la polisi lilichukua hatua ya kumtafuta mtuhumiwa na kufanikiwa kumkamata siku ya jana Novemba 16.

Alipohojiwa juu ya maandishi ya matusi katika barua alikiri na kudai kuwa anatambua kuwa ni makosa ndipo mtuhumiwa huyo akafunguliwa kesi ya kutoa lugha ya matusi na kufikishwa mahakamani na kasha kupatiwa hukumu hiyo.
Share To:

Post A Comment: