Monday, 8 November 2021

AGIZO LA WAZIRI AWESO LATEKELEZWA-RIDHIWANI


Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete, ameshukuru agizo la Waziri wa Maji Jumaa Aweso alilolitoa Novemba 6 mwaka huu ,kuwa ihakikishwe Pampu Za Maji Chamakweza na Msoga Zinawashwa limetekelezwa.

Aidha ameipongeza Serikali kwa mradi wa Maji Chalinze kukamilika kwa asilimia 98.

Akishukuru ujio wa Waziri wa maji Novemba 6, Ridhiwani alieleza mitambo ya kusukuma Maji imewashwa yote miwili kufuatia maelekezo ya Waziri wa Maji kuwa hadi kufika Novemba 7 mwaka huu Mchana na kazi zote zilizokuwa zimebaki ziwe zimemalizika.

Hata hivyo Waziri wa Maji alikagua na kuridhika kuruhusu maji yaanze kutumiwa na wananchi katika maeneo ya Chalinze ambapo miundombinu imekamilika. 

"Hizi ni habari njema kwa wananchi wa Chalinze ambao kwa muda mrefu wanahangaika na shida ya maji. "

Ridhiwani pia alimshukuru Hayati Rais John Magufuli kwa kuridhia kuanzisha mradi na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha anaukamilisha mradi huo.

#MajiNiUhai #ChalinzeMaji


No comments:

Post a Comment