Na Rhoda Simba, Dodoma.


WIZARA ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto imekutana  na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) pamoja  na Mashirika yasiyo ya kiserikali lengo likiwa  ni kuweza kushirikiana katika suala la kukabiliana na ugonjwa wa uviko 19.


Akizungumza na Waandishi wa habari  leo October 25 jijini hapa Katibu Mkuu  Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii jinsia Wazee na Watoto Profesa Abel Makubi amesema wao kama Serikali wametii agizo la Rais Samia Suluhu Hassan la kushirikiana na  mashirika yasiyo ya kiserikali kupambana na ugonjwa  wa uviko19.


‘’Wenzetu sekta binafsi walisema wapo tayari kukabiliana na vita hii  na wakasema maeneo ya kushirikiana ni kuongeza jitihada za kuwafikia wananchi kupata  chanjo hapo awali  tulishafikia kiwango cha kuchanja wananchi hadi elfu 50 kwa siku’’amesema Profesa Makubi


 


‘’Tuna kazi kubwa ya kuwatafuta wananchi kuchanja tumeona Serikali peke yetu hatuwezi tumeona ni bora tuwashirikishe Ngo’s mashirika ya kidini hata nyinyi waandishi wa habari tunataka wananchi wapate uelewa zaidi wa kuchanja’’


Pamoja na hayo pia amezungumzia kuhusu chanjo mpya ya sinopharm kwamba wananchi kwa sasa wanahitaji uelewa kuhusu chanjo hiyo kwani masharti yake ni kuchanja mara mbili na si mara moja kama ilivyokuwa kwa chanjo ya Jonson Jonson (JJ).


Nae Dkt Grace magembe Naibu katibu Mkuu  Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshugulikia afya amesema wanaendelea na  kampeni hiyo kwa kuwashirikisha  wananchi  katika mamlaka za serikali za mtaa  na mamalaka za mkoa na kama  ilivyo kazi ya ofisi ya tamisemi kushiriki kwao ni kuongoza afya na kutekeleza sera.


“Sisi TAMISEMI tuliandaa mkakati harakishi tulioelekeza katika wakuu wetu wa mkoa na wilaya kama unavyoona chanjo hii iliisha haraka kwasababu tuliwatumia viongozi husika na matokeo  tumeyaona kwasababu tuliweza kuwatumia viongozi wa Mtaa,Dini,hadi viongozi wa kimila”


Akizungumza kwa niaba ya wadau kutoka Baraza la Mashirika yasiyo ya Kiserikali (Nacongo)Dkt. Lilian Badi alisema,wao wapo tayari kushirikiana na Serikali katika kampeni ya kuhamasisha wananchi kwenda kupata chanjo ili kujikinga na maambukizi ya UVIKO 19.


Hata hivyo ametumia nafasi hiyo kuiomba Serikali iwawezeshe ili waweze kuifanya kazi hiyo ya kufikisha elimu kwa wananchi na kuikomboa nchi dhidi ya UVIKO 19.


“Sisi tunafanya kazi jamii na katika kampeni hii ya kuelimisha wananchi kwenda kupata chanjo ,tupo tayari kufanya kazi hii ila tunaiomba Serikali itupe ‘resouces’kwani uwezo wa kufikisha elimu kwa jamii tunao.”amesema Dkt.Badi

Share To:

Post A Comment: