Friday, 8 October 2021

WGNRR AFRIKA WAKABIDHI MSAADA WA VIFAA VYA UVIKO 19 KWA WENYE MAHITAJI MAALUM

Mkurugenzi wa WOMEN'S GLOBAL NETWORK FOR REPRODUCTIVE RIGHT AFRICA (WGNRR), Bwana Nondo Raymond akikabidhi msaada wa vifaa vya kupambana na Uviko 19 na mahitaji muhimu ya afya ya uzazi kwa taasisi ya sauti ya wanawake wenye ulemavu ( SWAUTA).


Bi. Stella Jailos mkurugenzi wa sauti ya wanawake wenye ulemavu Tanzania (SWAUTA) na Afisa Mtendaji wa kata ya Mwananyamala Ngatumbura Mickdad wakikabidhiwa msaada wa vifaa vya kupambana na Uviko 19 na mahitaji muhimu ya afya ya uzazi na mkurugenzi wa WGNRR


Msaada wa vifaa vya kupambana na Uviko 19 na mahitaji muhimu ya afya ya uzazi vilivyotolewa kwa taasisi ya sauti ya wanawake wenye ulemavu ( SWAUTA) Vyenye thamani ya shilingi milioni 11.


Baadhi ya wanachama wa SWAUTI wakisikiliza hotuba ya mkurugenzi wa WGNRR Bwana Nondo Raymond
Afisa Mtendaji wa kata ya Mwananyamala Ngatumbura Mickdad akipokea msaada wa vifaa vya kupambana na Uviko 19 na mahitaji muhimu ya afya ya uzazi.


******************************


Na James Salvatory


SERIKALI yaombwa kuweka mkakati jumuishi katika mapambano dhidi ya Uviko 19 hususani kujumuisha watu wenye uhitaji maalum Nchini.


Rai hiyo imetolewa jana Oktoba 07,2021 jijini Dar es salaam, na Mkurugenzi wa WOMEN'S GLOBAL NETWORK FOR REPRODUCTIVE RIGHT AFRICA (WGNRR), Bwana Nondo Raymond wakati wakikabidhi msaada wa vifaa vya kupambana na Uviko 19 na mahitaji muhimu ya afya ya uzazi kwa taasisi ya sauti ya wanawake wenye ulemavu ( SWAUTA) Vyenye thamani ya shilingi milioni 11.


Nondo amesema kuwa watu wenye mahitaji maalumu wanapitia changamoto nyingi ikiwemo kutokupata taarifa sahihi za afya ya uzazi, kutojumuishwa katika mipango na mikakati inayochukuliwa ya kupambana na Uviko 19.


"Changamoto zingine ni vitendea kazi vya kujikinga mara nyingi kutokuzingatia mahitaji yao, kushindwa kumudu gharama za vifaa vya kujinga pamoja na kukosa taarifa sahihi za kujilinda na covid 19"amesema


"Kwa sababu hiyo tumefikiria ni vizuri kuleta msaada katika taasisi hii inaojumuisha taarifa na vifaa muhimu vitakavyowasaidia"amesema Nondo.


Aidha amesema kuwa wamekabidhi Vitakasa mikono katoni 64,Taulo za kike (Pads) 410,Barakoa 650, Sabuni za kunawa 64 , Kopo 100 za vitamini C pamoja na vijitabu vyenye taarifa ya Nukta nundu 75.


Katika hatua nyingine amesema kuwa suala la Uviko 19 lisisahaulishe mahitaji ya afya ya uzazi kwa watu wenye mahitaji maalum.


Kwa upande wake muweka Hazina wa Taasisi iliyopewa misaada huo ya SWAUTA Bi Adelina Muluge ameishukuru WGNRR kwa Msaada huo kwani wao wamekuwa wakisahaulika katika katika baadhi ya mambo ikiwemo mapambano dhidi ya Uviko 19.

"sisi wanawake tuna mahitaji mengi hususan sisi wenye mahitaji maalum tuna uhitaji mara mbili yake hivyo msaada huo utakuwa msaada kwetu kwa sababu tunaachwa nyuma mara nyingi pia msaada huu usiishie hapa uendelee na kwa mambo mengine"amesema


Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Mwananyamala Ngatumbura Mickdadm amesema kuwa utolewaji wa msaada huo kwa watu wenye ulemavu utakwenda kuwasaidia wahitaji katika maisha yao ya kila siku.

No comments:

Post a Comment