Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba na ujumbe aliombatana nao wakisindikizwa na wenyeji wao baada ya kufanya kikao na ziara katika ofisi za ADNOC, Abu Dhabi.

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa ADNOC Global Trading Ltd, Ndg. Ahmed Bin Thalith. Wengine pichani wanaofuatilia mazungumzo hayo ni Balozi wa Tanzania UAE, Balozi Mohamed Mtonga (wa tatu kulia), Kamishna wa Petroli na Mafuta kutoka Wizara ya Nishati Tanzania, Ndg. Michael Mjinja (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa kwanza kulia)

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba akizungumza jambo na Mkurugenzi Mkuu wa ADNOC Global Trading Ltd, Ndg. Ahmed Bin Thalith wakati wa kutembelea ofisi za ADNOC kujionea namna wanavyoendesha na kusimamia biashara ya mafuta. Wengine pichani ni Kamishna wa Petroli na Mafuta, Ndg. Michael Mjinja (wa pili kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio (wa tatu kulia)


 Abu Dhabi, Umoja wa Falme za Kiarabu

Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba ambaye anaendelea na ziara yake ya kikazi Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amekutana na kufanya mazungumzo na Kampuni ya Mafuta ya Taifa ya Abu Dhabi (ADNOC). 

Waziri Makamba amefanya kikao hicho tarehe 25 Oktoba 2021 na Mkurugenzi Mkuu wa ADNOC Global Trading Ltd, Ndg. Ahmed Bin Thalith ambapo walijadili masuala mbalimbali ikiwemo kudumisha uhusiano baina ya Tanzania na Abu Dhabi katika sekta ya mafuta na gesi. 

Waziri Makamba pia alipata nafasi ya kutembelea ofisi za ADNOC na kujionea matumizi ya hali ya juu ya teknolojia katika kuendesha na kusimamia biashara ya mafuta. “Tanzania tuna nafasi kubwa ya kujifunza kutoka kwa wenzetu kama Adu Dhabi ambao wamekuwepo katika sekta ya mafuta na gesi kwa muda mrefu na ziara hii ni sehemu ya kujifunza huko” alisema Waziri Makamba.

Waziri Makamba aliambatana na Balozi wa Tanzania nchini UAE Balozi Mohamed Mtonga, Kamishna wa Petroli na Mafuta kutoka Wizara ya Nishati Tanzania, Ndg. Michael Mjinja na Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio.

Share To:

Post A Comment: