Wanafunzi na Walimu wa shule ya sekondari ya wavulana kidato cha tano na sita Pamoja wameilalamikia serikali kuisahau shule hiyo katika mambo mbalimbali huku ikikabiliwa na changamoto lukuki zikiwemo za uhaba wa madarasa ,jengo la utawala,nyumba za walimu ,bwalo , mabweni pamoja na maktaba.

Wakizungumza  shuleni hapo wanafunzi wa kidato cha tano na sita pamoja na walimu wao walisema shule hiyo imesahaulika na serikali licha ya kuwa na changamoto lukuki za uhaba wa madarasa ,mabweni ,bwalo ,nyumba za walimu pamoja na jengo la utawala .

Makamu mkuu wa shule hiyo bwana John Ndunguru alikiri kuwepo kwa mapungufu hayo lakini kila mwaka taarifa za upungufu na changamoto za shule hizo zinapelekwa katika ofisi ya mkurugenzi kwa hatua Zaidi

Aidha Ndunguru alisema shule hiyo ilijengwa kwa michango kutoka Halmashauri za mkoa wa Ruvuma kwa maana ya shule ya wavulana ya mkoa wa Ruvuma kidato cha tano na sita na mwaka huu mwezi aprili shule hiyo imekabidhiwa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo.

Ndunguru alidai jitihada za shule kuomba wadau kuisaidia shule hiyo ilifanikiwa kwa kampuni ya Mantra Tanzania limited kuwajengea maabara kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi hao waweze kupata elimu bora huku nyumba moja ya mwalimu ikitumika kama jengo la utawala.

Mwanafunzi wa kidato cha sita bwana Fadhili Makanga alisema kuwa shule yao imesahaulika sana huku akiitaja shule ya sekondari ya Nasuli kupendelewa kwa kila kitu na wao kusahaulika kwa kila kitu katika shule yao.

Roza Nabahani afisa elimu shule za sekondari Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alipoulizwa kuhusu kuisaidia shule hiyo kupitia fedha zilizotolewa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua changamoto inayoikabili shule hiyo alisema fedha zilizotolewa na serikali ni kwa ajili ya kutatua changamoto ya wanafunzi wa kidato cha kwanza shule ya sekondari ya Pamoja haina kidato cha kwanza ,hivyo tunaendelea kutafuta fedha ili kutatua changamoto zilizopo katika shule hiyo alisema Nabahani.

Amos Kanige afisa mipango wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo amedai shule hiyo imeingizwa katika bajeti ya 2021/2022 kujenga madarasa ,mabweni pamoja na kuzitumia fedha zilizotolewa na Raisi wa Jamhuri ya Muungano Samia Suluhu Hassan kutatua changamoto za miundombinu zinazowakabili wanafunzi wa shule hiyo kwa sasa.

Kanige alitaja changamoto ya hivi karibuni ambayo shule hiyo ilikumbana nayo ya uhaba wa chakula Halmashauri ililetewa taarifa ya tatizo hilo na ofisi ya Mkurugenzi ilichukua jukumu la kuhakikisha chakula kinanunuliwa na ofisi ilifanya hivyo.

Shule ya sekondari Pamoja ilifunguliwa tarehe 21mwezi februali 2011 ,kwa sasa shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 196 ikiwa kidato cha tano 114 na kidato cha sita 82 walimu 14 wanaume 11 na wanawake 3 na inakabiliwa na upungufu wa miundombinu ya madarasa,mabweni,nyumba za walimu pamoja na jengo la utawala.
Share To:

Post A Comment: