Na Woinde Shizza, ARUSHA


Mkuu wa chuo cha uhasibu Arusha,Profesa Eliaman Sedoyeka amewataka vijana kutumia Teknolojia ya habari na Mawasiliano kujiajiri ili kujikwamua kiuchumi.



Akizungumza kando ya mkutano wa tano wa mwaka wa Tehama nchini unaofanyika  jijini Arusha,Profesa Sedoyeka alisema vijana watumie Tehama kwa kujiajiri kwani ni sehemu  yenye fursa zaidi ya maeneo mengine.



"Ukiangalia IT ni eneo ambalo ni rahisi sana kujiajiri ikiwa hata mtaji wake wa kujiajiri ni mdogo  kwani ukinzia upigaji wa picha na video ni sehemu ya Tehama,"alisema Prof.Sedoyeka.




 Sambamba na hilo alisema pamoja na chuo hicho kujikita katika mambo ya uhasibu na fedha kutokana na mabadiliko ya dunia wameongeza kozi mbalimbali zinazohusiana na Tehama kama Sayansi ya Komputer ili kuwasaidia vijana katika kujiajiri wenyewe na kujikwamua kiuchumi.



"Hivyo tumejikuta tumekuwa kutokana na chuo chetu kuwa chini ya wizara fedha nakuwa na majukumu ya kuhakikisha tunatoa wataalamu wanaosomea sekta ya fedha na Tehama kwa ujumla lakini pamoja na maonyesho haya watu watapata fursa ya kujionea fursa kutokana na vijana wa chuo cha uhasibu Arusha wanazofanya kwa vitendo zaidi,"alisema Profesa Sedoyeka.



Alisema katika mkutano huo alitoa mada inayohusiana  na namna ya walivyojiandaa walivyokabiliana na janga la ugonjwa wa covid-19 nakutoa uzoefu wa walivyotumia teknolojia ya Teham katika kufundisha wanafunzi nakuweza kufikia lengo la wanafunzi kusomoa kwa kutumia njia mbalimbali.



"Njia hizo ni pamoja nakutumia zoom katika ufundishaji na baada ya kufungua chuo waliendelea kutumia mfumo wa ufundishaji kwa njia ya Teknolojia za Tehama yaani kusoma kwa njia mtando kwa walio nje ya Arusha,"alisema Sedoyeka.



Profesa alisema dhana ya kusoma kwa mtandao haikuanza zama hizi bali ilikuwepo katika kipindi kirefu kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wanasoma kwa njia ya vipindi vya redio na baadaye ikaja njia ya posta na intaneti ilivyoingia ndipo mawazo mbali yakaja katika kumuwezesha mtu yeyote kusoma popote kule alipo.




Aidha Mkuu huyo alisema lengo la chuo hicho ni kuwaandaa vijana kuanzisha makampuni yao ya Tehama nakuweza kuajiri wengine.

Share To:

Post A Comment: