Monday, 18 October 2021

RAISI SAMIA AKAGUA KITUO NO.5 CHA KUSUKUMIA MAJI ARUSHA IKIWA NI SEHEMU YA MRADI MKUBWA WA MAJI WA BIL.520


Rais Samia Suluhu Hassan katikati akikata utepe Ishara ya uzinduzi wa hospitali ya wilaya Njiro Jijini Arusha,kushoto kwake ni waziri wa Tamisemi Ummy Mwalimu,Mkuu wa mkoa wa Arusha John Mongela na mbunge wa Arusha Mrisho Gambo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mmoja wa akina mama kati waliojifungua katika hospital ya wilaya aliyoizindua leo up 17/10/2021 Jijini Arusha iliyojengwa kwa tsh bil.2.5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akisalimiana na mmoja wa akina mama kati waliojifungua katika hospital ya wilaya aliyoizindua leo 17/10/2021 Jijini Arusha iliyojengwa kwa tsh bil.2.5
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi hundi kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu wa kata ya Themi Njiro Jijini Arusha ya shilingi mil.387,380,615 (NMB)mara  baada ya   kuzindua hospital ya wilaya  leo 17/10/2021 Jijini Arusha  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akimkabidhi hundi kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu wa kata ya Themi Njiro Jijini Arusha ya shilingi mil. 661,852,000( NBC)mara  baada ya   kuzindua hospitali ya wilaya   17/10/2021 Jijini Arusha  
Wananchi wakimshangilia Rais Samia Suluhu alipokuwa akihutubia leo Jijini ArushaRais wa Jamhuri ya Tanzania Samia Suluhu Hassan, amekagua Kituo na 5 Cha kusukumia maji maeneo ya chekereni ikiwa ni sehemu ya mradi mkubwa wa maji wa bil.520 ,katika eneo la ARUMERU  na Jiji la Arusha,ambapo ni mradi wa pili wa maji kwa ukubwa nchini Tanzania baada ya mradi wa maji uliopo mkoa wa Tabora

Akizungumza na wananchi kata ya Mlangarini wilaya ya Arumeru, Rais Samia alisema kuwa changamoto kubwa ya jiji la Arusha ilikuwa maji na barabara ,ambapo maji wameshautatua kupitia mradi utakaokamilika mwakani,na kusema suala  la barabara watakaa na Uongozi wa mkoa pamoja na Tanrod /Tarura ,kuangalia ni sehemu gani kuna changamoto

" Lengo la Serikali ni kuunganisha barabara za wilaya.alisema Samia.

Akitoa taarifa ya Maendeleo ya mradi huo Mkurugenzi mtendaji wa (AWSA)Justine Rujomba ,alisema kuwa Kituo hicho kina uwezo wa kupitisha maji lita mil.80,000 ambapo wameweza kuchimba kutoka hai Umbali wa km 83, ambapo katika vijiji mradi huo utapitia navyo vitanufaika kwa kupata maji 

Rujoba alisema kuwa chanzo kikubwa Cha maji ni visima virefu katika maeneo mbalimbali, ambapo wamechimba visima 18 kutoka eneo la majimoto hai , ni km 83 hadi mredi ulipo, na maji yake siyo ya chumvi ,hadi Sasa imekamilika kwa 75% unategemewa kukamilika June mwakani 2022

Mradi wa Chekereni unavisima 41 na tenki la maji lenye ujazo wa lita milioni 3 pamoja na pampu za kusukuma maji.

Wakati huohuo Rais Samia Suluhu Hassan alizindua hospital ya wilaya kata ya njiro lililogarimu kiasi Cha Shi Bil.2.5, sambamba na  kukabidhi hundi za mikopo kwa wanawake,vijana na watu wenye ulemavu wenye jumla ya sh.bil.1.3

Baadhi ya wakazi watakaonufaika na mradi huo wameishukuru serikali ,kwani karibuni wataanza kupata maji safi na salama, ambayo hayatakuwa na athari za kiafya, kama kuharibu rangi ya meno yao.

Raia Samia anaendelea na ziara yake mkoani Arusha ambapo aliwasili jana jioni akitokea mkoa wa Kilimanjaro.

No comments:

Post a Comment