Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 unatarajiwa kuanza siku ya Jumatatu tarehe 25 Oktoba 2021 na kumalizika tarehe 12 Novemba 2021 Jijini Dodoma. 

Mkutano huu utapokea, utajadili na kutolea uamuzi Rufaa na Malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa Tume na Watumishi wa Umma ambao hawakuridhika na uamuzi uliotolewa na Waajiri, Mamlaka za Ajira na Mamlaka zao za Nidhamu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu wa Tume, Bw. Mathew M. Kirama, Mkutano huu utaongozwa na Mwenyekiti wa Tume Mheshimiwa Jaji  Rufaa (Mst.) Dkt. Steven J. Bwana. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni Kujadili taarifa mbalimbali za utekelezaji wa Majukumu ya Tume na Mpango Mkakati  wa Tume ya Utumishi wa Umma kwa kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi 2025/2026.

Share To:

Post A Comment: