Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere. Kushoto ni Waziri wa Nishati, January Makamba na kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.


Waziri wa Nishati, January Makamba (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kumalizika kwa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (katikati) katika mradi wa umeme wa Julius Nyerere. Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (wa Tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati na Wakuu wa mikoa ya Morogoro na Pwani mara baada ya kumaliza kikao cha majumuisho kilichofanyika katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere. Wa Tatu kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango, Wa Nne kushoto ni Waziri wa Nishati, January Makamba, Wa Pili kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (wa Tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka TANESCO na Wakuu wa mikoa ya Morogoro na Pwani mara baada ya kumaliza kikao cha majumuisho kilichofanyika katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere. Wa Tatu kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango, Wa Nne kushoto ni Waziri wa Nishati, January Makamba, Wa Pili kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato na wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali.


Watendaji mbalimbali kutoka Wizara ya Nishati, TANESCO, Mkoa wa Morogoro na Pwani, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (hayupo pichani) wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere.


'Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (wa Tano kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali kutoka, Wizara ya Nishati, TANESCO na Wakuu wa mikoa ya Morogoro na Pwani mara baada ya kumaliza kikao cha majumuisho kilichofanyika katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere. Wa Tatu kulia ni Mke wa Makamu wa Rais, Mbonimpaye Mpango, Wa Nne kushoto ni Waziri wa Nishati, January Makamba, Wa Pili kulia ni Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, wa kwanza kulia ni Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Nishati, Kheri Mahimbali, Wa Nne kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, Wa Tatu kushoto Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigellah na Wa Pili kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Philip Isdor Mpango (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho mara baada ya kumaliza ziara yake katika mradi wa Umeme wa Julius Nyerere

.............................................................................

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Philip Isdor Mpango ametoa maelekezo mbalimbali kwa Wizara ya Nishati na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) yatakayoboresha utekelezaji Mradi wa Bwawa la Kufua Umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ili kuweza kukamilika kwa wakati uliopangwa.

Maelekezo hayo ameyatoa tarehe 13 Oktoba, 2021 wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku mbili ya kutembelea mradi wa JNHPP kilichofanyika katika eneo la Mradi na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Waziri wa Nishati, January Makamba.

Ameelekeza kuwa, Katibu Mkuu Kiongozi kuteua timu ya wataalam kutoka Wizara mbalimbali, baadhi ya taasisi za Serikali na vyombo vya Ulinzi na Usalama itakayochambua changamoto mbalimbali zinazohusu mradi huo na kupendekeza utatuzi wake.

“Timu ya hiyo ya Serikali ichambue changamoto hizo na kupendekeza ushauri wake, ikiwemo suala la ujenzi wa njia ya kusafirisha umeme kutoka eneo la mradi hadi mji wa Chalinze na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme,” alibainisha Makamu wa Rais

Alisisitiza kuwa, TANESCO ijenge njia ya kusafirisha umeme kutoka eneo hilo la mradi kwenda Chalinze na ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Chalinze ili kuwezesha majaribio ya kuzalisha umeme mara mradi utakapokamilika.

Maelekezo mengine ni pamoja na TANESCO kuwa na wataalam wa kutosha katika nyanja mbalimbali ikiwemo Wahandisi, Wanasheria, Wasanifu na Wahandisi wa mabwawa ya kufua umeme watakaowezesha Shirika hilo kufanya kazi kwa ufanisi ikiwemo ya usimamizi wa mradi huo.

“Angalieni uwezekano wa kuongeza wataalam sehemu zenye mapungufu, mkandarasi aongeze vitendea kazi vinavyohitajika, na pia muda wa kufanya kazi uangaliwe ili mradi huu ufanikiwe.” amesisitiza Makamu wa Rais.

Pia, alimuelekeza Waziri wa Nishati kufuatilia masuala yanayohusu fedha zinazotengwa kwa ajili ya Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) ili yafanyike kwa ufanisi.

Kwa upande mwingine, ameilekeza Wizara ya Nishati, TANESCO na mkandarasi wa mradi kukutana ili kujadili namna ya kufidia muda uliopotea kutokana na sababu mbalimbali katika utekelezaji wa mradi huo.

Aliongeza kuagiza kuwa, Ofisi ya Waziri Mkuu kusaidia kuharakishwa kwa upatikanaji wa vibali vya wataalam kutoka nje ya nchi wanaoingia nchini kufanya kazi kwenye mradi huo.

Kwa upande wake, Waziri wa Nishati, January Makamba alimshukuru Makamu wa Rais kwa kutembelea mradi wa JNHPP na kutoa maelekezo hayo na kuahidi kuanza kuyafanyia kazi mara moja.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria kikao hicho cha majumuisho ni pamoja na Naibu Waziri wa Nishati, Wakili Stephen Byabato, Naibu Katibu Mkuu, Kheri Mahimbali, Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakar Kunenge, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Martin Shigellah, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Maharage Chande na watendaji wengine kutoka Wizara ya Nishati na TANESCO.

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: