Mradi wa upanuzi wa barabara ya Morogoro sehemu ya Kimara-Kibaha kwa njia nane (Km 19.2), unaendelea vizuri na kwa sasa umefika asilimia 94

Mradi huu unafadhiliwa na Serikali kwa asilimia mia moja na gharama yake ni takriban Shilingi Bilioni 161 ukitarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba nwaka huu.

Aidha, Serikali imeshamlipa Mkandarasi malipo ya zaidi ya Shilingi bilioni 149. 8 ambazo ni sawa na asilimia 93 kulingana na kazi aliyoifanya.

Hadi sasa kazi zilizobakia zikiwa ni kuweka taa za kuongozea magari, Taa za kuangaza barabarani, kuweka kingo (kerbstobne) na kutenga njia zinazoelekea mjini na zinazotoka mjini na kumalizia lami kipande cha kilometa 4 kutoka eneo la Gogoni- Kibamba hadi Kibaha.

Mradi huu unatekelezwa na Serikali kupitia Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), ambapo lengo lake kubwa ni kupunguza msongamano kwa wasafiri na wasafirishaji wanaongia katikati ya jiji la Dar es Salaam.

kukamilika kwa mradi huu kutaunganisha nchi yetu na nchi jirani za Rwanda, Burundi, Congo na Malawi.

Mradi huu ulianza mwaka 2018 na unajengwa na Kampuni ya kikandarasi ya Estim kutoka Tanzania.

Share To:

Post A Comment: