MKUU wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani kushoto ni Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Spora Liana ,Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo akifuatiwa na Naibu Meya wa Jiji hilo Calvas Joseph
Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurhamani Shiloo akizungumza wakati wa kikao hicho kushoto ni Naibu Meya wake Calvas Joseph akiwfuatiwa na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga Meja Mkoba
MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Spora Liana akizungumza wakati wa kikao hicho
DIWANI wa Kata ya Chumbageni Ernest Kimaya akiuliza swali wakati wa kikao hicho


NA OSCAR ASSENGA,TANGA

Mkuu wa wilaya ya Tanga Hashim Mgandilwa ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha biashara ya madanguro maarufu kama madada poa inakoma mara moja Jijini humo
 
DC Mganndilwa alitoa agizo hilo wakati wa  kikao cha cha baraza la madiwani wa halamashauri ya jiji la Tanga ambapo aliyataja maeneo hayo kuwa ni  Sabasaba na barabara ya Uhuru na kusema kuwa  wanaofanya biashara kwenye maeneo hayo watafute miji mingine. 

"Kuna maeneo kwetu sisi bado kuna, madanguro ambayo dada zetu wanajiuza naomba nitumie hadhara hii kwakuwa vyombo vya dola vipo hapa niwaombe tuanze kushughulika na hawa watu natamani tuone mji wetu unakuwa safi hatutaki kuona hizi biashara za kujiuza jeshi la polisi wakati nikifanya opereshen zenu basi mshughulike na watu hawa, "alisistiza DC Mgandilwa. 

Katika hatua nyingine Mgandilwa amesema pamoja na hayo analipongeza jiji hilo kwa kuweza kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi na kutaka kuwalipa fidia wananchi ambao bado wana migogoro ya fidia zao lengo ni kuondokana na migogoro isiyokuwa na lazima.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa jiji la Tanga Abdulrahman Shiloo amewataka wakuu wa idara kuheshimu maamuzi yanayofanywa na baraza la madiwani ili kuepukana na migongano isiyokuwa ya lazima inayoweza kukwamisha jitihada za maendeleo kwenye jiji hilo. 

"Nitoe angalizo kwa wakuu wetu wa idara na watumishi wote wa halmashauri wapatao 3000 waelewe kwamba kikao cha mwisho chenye maamuzi katika jiji hili ni baraza la madiwani hivyo wasijaribu wala wasiwaze kujikweza kimadaraka hakikisheni sheria kanuni taratibu na miongozo zinafuatwa ili tusifikie kwenye migongano, "alisistiza Meya Shiloo. 

Mkurugenzi wa jiji la Tanga Spora Liana amesema Halmashauri hiyo itatoa taarifa ya kila matumizi ya fedha yanayofanywa kwa wananchi lengo ni kuweka wazi kwa kila mwananchi kufahamu fedha za maendeleo zinazotolewa kwenye maeneo yao. 

Mwisho.
Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: