Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Picha iliyosambaa kwenye mitandao ya kijamii  ikionyesha watoto wakivuka kwenye kidaraja hatarishi ni ya zamani miaka minne iliyopita na hapo ni Kijiji cha Ibanda, Kata ya Urekingombe Tarafa ya Mikumi Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa.


Kijiji hicho kiko umbali wa Kilomita 180 kutoka Makao Makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa


Serikali ilishachukua hatua kupitia Wakala wa barabara za vijijini na mijini (TARURA) kwa kujenga daraja la muda la waenda kwa miguu ambalo ni la mbao.


 Kwa sasa TARURA inajenga daraja la kudumu (Cable stay suspension pedestrian bridge) litakaliwezesha waenda kwa miguu  na boda boda kupita. Kazi hii itakamikika Mwezi Dec 2021  itagharimu takribani shilingi Mil 80.


Tunajali  changamoto za wananchi wetu na tunazitatua kadri rasilimali zinavyopatikana.

Share To:

Post A Comment: