Friday, 1 October 2021

Benki ya CRDB yaingia mkataba na Chuo Kikuu cha Dodoma wa ujenzi wa jengo la kisasa la kutolea huduma katika lango kuu la chuo hicho

 

Benki ya CRDB yaingia mkataba na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) wa ujenzi wa jengo la kisasa la kutolea huduma katika lango kuu la chuo hicho.
Jengo hilo (mchoro pichani) ambalo linatarajiwa kugharimu shilingi milioni 150, litakuwa kituo cha huduma za kisasa za Benki ya CRDB, ATMs na skrini za kielektoniki zitakazokuwa na matangazo ya huduma zitolewazo na benki pamoja na huduma za kujihudumia (Self Service). 
Huduma nyingine zitakazotolewa ni pamoja na zile za Chuo Kikuu cha Dodoma kama za usalama, maelekezo kwa wageni wa chuo, na banda la ulinzi

No comments:

Post a Comment