Na Rhoda Simba Dodoma

 Asasi za Kiraia nchini  AZAKI zimetakiwa kuona umuhimu wa maendeleo  ya watu nchini ili kuepuka kuwa na maendeleo ya vitu wakati watu masikini.


Akizungumza leo  october 25 jijini hapa  Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation For Civil Society (FCS) Francis Kiwanga wakati wa mjadala wa kujadili  nini mchango wa Asasi za kiraia kwa jamii pamoja na utoaji mchango wa Masaada wa kisheria kwa jamii.

Kiwanga akizungumza katika mjadala huo amesema kuwa pamoja na Azaki kufanya kazi vizuri na kuwa karibu na taasisi za Serikali lakini Azaki zinatakiwa kuona umuhimu wa maendeleo ya watu na siyo vitu kwani unaweza kuwa na maendeleo  ya vitu huku watu masikini.

"Nataka kuwapa mfano kuna wakati nilikuwa nasafiri kutoka Bukoba kwenda Mwanza kwa basi lakini nilikutana na masoko mazuri cha kushangaza hayakuwa na watu sasa tusijivunie namba za vitu bali maendeleo ya watu" amesema.

Kwa upande wake Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Anna Henga amesema wananchi  Serikali inawekeza sana lakini miradi mingi lakini  haidumu Kwa kuwa wananchi Wengi hawana mwamko wa maendeleo Kutokana na dhana ya umaskini inayowakabili.

Amesema ,wananchi wasipokuwa na uwezo hawawezi kutambua thamani ya miradi na kushindwa kuitunza

"Tunapaswa kutumia muda wetu mwingi kiwaelewesha Wananchi kuhusu maana ya maendeleo na umuhimu wake ili nao wapate kushiriki ujenzi wa maendeleo kwa vitendo,"ameeleza.

Licha ya hayo Henga ameeleza kuwa umaskini usipo tibiwa itaendelea kuwa kidonda Kwa jamii ambapo  karibu asilimia 50 ya watoto waishio mitaani wanatokana  na ndoa zilizovunjika Kutokana na ugumu wa maisha.

"Tunataka kupambana na umaskini uliopitiliza,tunasaidia   jamii  msaada wa kisheria pale wanapokuwa wamekwama na wakati mwingine kukosa uwezo wa kumpata wakili Kwa kukosa fedha,hivyo ndivyo tunapambana walau kuiokoa jamii"amefafanua.

Pamoja na mambo mengine  ametolea mfano wa mmoja wa mwanamke ambaye alitumia muda wa miaka 40 kufuatilia mgogoro wa shamba lakini baada ya yeye kuingilia kati aliweza kufanikiwa kupata haki yake ya shamba kwa muda mfupi.

"Kesi nyingi zinatumia muda mwingi nyingine zinakuwa na mazingira ya rushwa,Lazima tuokatae rushwa ,rushwa ni umaskini, tunatamani Kila mwananchi aelewe haki zake kisheria na hii itasaidia kuleta maendeleo na kumaliza kero ya kesi ndogo za kawaida kabisa zilizokuwa zikichukua miaka 2 hadi 4 kumalizika haraka,"alifafanua Mwanasheria huyo.

"Tumebaini kuwa kesi nyingi ni za migogoro ya mashamba (ardhi),migogoro ya mirathi,migogoro ya ajira  na migogoro ya ndoa zilizovunjika,karibia asilimia 50 ya watoto wanaoishi mitaani wanatokana na ndoa zilizovunjika, tumekuwa tukitoa elimu kwenye mabaraza ya ndoa,kutunga sera ya mabaraza ya ndoa kwa kushirikiana na wizara husika kumaliza janga hili,"ameeleza Henga.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Jukwaa Huru la Kilimo Nchini( ANSAF), Audax Rukonge akichangia mjadala huo wa Mchango wa Azaki kwa jamii na ni nini kifanyike amesema,Asasi za kiraia zinatakiwa kujenga tabia ya kuaminiana ili kuleta mashirikiano.

Amesema, pamoja na kujenga  tabia ya kuaminiana bado Asasi hizo zinatakiwa kuwa na mawazo ya pamoja na kuwa na uwazi kwa kile wanachokifanya.

Akichangia katika mjadala huo pia amesema kuwa ili asasi ziweze kufanya vizuri nilazima zijenge utamaduni wa kuwa na maono ya pamoja,vipaumbele vya pamoja,utekelezaji wa pamoja na kuwa na mifumo ya uwajibikaji wa  pamoja.
Share To:

Post A Comment: