Na Angela Msimbira KISARAWE


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe Ummy  amemtaka Mhandisi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe  Ashraf  Bige  kujitathmini kwakukubali  kuwa ameridhishwa. na Ujenzi licha ya kuwepo kwa mapungufu katika ujenzi wa Hospitali ya Wilaya hiyo


Akikagua ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kisarawe leo Waziri Ummy amesema ameridhishwa na Maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo lakini Halmashauri ihakikishe inasimamia mapungufu yaliojitokeza na kuhakikisha wanakamilisha ujenzi kwa wakati


Waziri Ummy amesema kuwa hajaridhishwa na utendaji kazi wa muhandisi huyo kwa kuwa hajatimiza wajibu wake kikamilifu katika usimamizi wa ujenzi wa Hospitali hiyo kwa kuwa kumekuwwpo namapungufu mengi katika ujenzi huo

"Haiwezekani milango ikatofautiana na kusababisha muonekano wa jengo kuwa mbaya halafu Mhandisi anasema ameridhishwa na Ujenzi, na kuagiza ujitathmini kama anatosha katika nafasi yako" amesisitiza Waziri Ummy


Aidha umemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani kumpeleka taarifa kuhusu utendaji kazi wa Mhandisi huyo ili aweze kuchukuliwa hatua za kinidhamu kwa kuwa ndio mshauri Mkuu wa ujenzi huo

Share To:

TANGA RAHA BLOG

Post A Comment: