Saturday, 25 September 2021

WAZIRI BITEKO AWATAKA WACHIMBAJI NA WAFANYABIASHRA WA TANZANITE KUWA WAMOJA

 


Waziri wa madini Dotto Biteko amewataka wachimbaji wadogo na wakubwa wa madini ya Tanzanite pamoja na wafanyabiashara wa madini kuwa na umoja katika kuiwezesha biashara hiyo kukuwa na kuleta maendeleo nchini.


Akizungumza katika kikao na wadau hao Biteko amesema sekta ya madini ni sekta ambayo inapaswa kuonekana ikikuwa na kuleta maendeleo kwa wazawa.


Aidha akizungumzia suala la uhamishaji wa soko la madini lililopo Mkoani Arusha,Biteko amesema kuwa uhamishwaji huo hautaleta madhara yoyote kwani uwepo wa soko katika mji mdogo wa mererani kutaleta maendeleo kwa wakazi wa mji wa mererani kunufaika na madini hayo.


"Sekta hii ya madini tumeifikisha hapa ilipo kwasababu wadau wasema na sisi serikali  tunachukuwa tunafanyia kazi kwa kuangalia maslahi mapana ya nchi."Alisema Waziri Biteko


Awali Waziri Biteko akitembelea soko la madini lililopo katika Mji huo ameagiza kuwepo kwa uwekaji wa taarifa sahihi katika mfumo wa lieletroniki utakao onyesha taarifa za uuzaji na uuzaji wa madini ya Tanzanite ili kuweza kuepuka mkanganyiko na upotevu wa taarifa.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Simanjiro Christopher Ole Sendeka anesema kuwa ipo haja kwa wizara kuweka utaaratibu wa ufanyaji wa biashara za madini yanayozidi gramu 2 kwa kuweka mapendekezo ya ujazaji wa fomu itakayoonyesha uuzaji wa madini kufanyika kutoka kwa dila kwenda kwa broker.


"Naomba nipendekeze Mhe.Waziri mtu akitoka na madini yake kuandaliwe fomu itakayotoa wajibu kwake ya kuthibitisha gram halisi za madini yanayoensa kuuzwa na idadi ya madini yaliyouzwa kwa mtu yupi ili tukitaka kufuatilia iwe rahisi lakini biashara hiyo ikifanyika Mererani."Alisema Ole Sendeka


Ameongwza kwa kuwataka wafanyabiashara na wachimbaji wa madini hayo kuipensa nchi na kuwa wazalendo wa nchi yao wenyewe kwa kuzuia wizi na utoroshwaji wa madini ya Tanzanite na kuahidi kuendelea kuishawishi serikali kuendelea kutenga fedha kwaajili ya ujenzi katika eneo la  APZA nila kuwakwaza wachecha wenye nia ya kujenga ofisi zao wenyewe.


Naye Mwenyekiti wa chama cha wafanyabiashara wa madini Tanzania TAMIDA Bwn.Sammy Mollel katika kikao hicho ameomba kuondolewa kwa  VAT kati ya mchimbaji na mchimbaji kwani kwa kufanya hivyo kutarudisha nyuma biashara ya madini pamoja na kupunguzwa kwa idadi ya leseni zilizopo na kuwa na leseni moja. 


"Serikali ilishaamua wafanyabiashara kuhama nao hawana chaguo ambaye atashindwa kuhamia Mererani muda ukiisha anyimwe leseni kwani siku 90 zinatosha kudhibitisha ambao wataweza kuhamia na ambao watashindwa ambapo alisema hadi hivi sasa wafanyabiashara zaidi ya 50 wameshafungua ofisi katika eneo hilo.Mkuu wa Mkoa wa Mererani Makongoro Nyerere katika kikao hicho 


Ameongeza kuwa suala la wafanyabiashara wa madini kuhamia katika mji mdogo wa Mererani hakuna aliyekataa lakini wakiweka miundombinu kila mmoja atahamia na kuendelea kufanya biashara yake.Nao baadhi ya viongozi wa uchimbaji wa madini na vito vya Tanzanite Mererani Amani Yusufu ambaye ni mwenyekiti wa tanzanite amesema madini ya tanzanite yameshuka bei kutokana na mutokuwepo kwa nguvu ya uchumi katika mfuko hivyo ameiomba serikali kutengeneza mfumo rafiki utakao msaidia mchimbaji kuwa na nguvu na dhamani ya kole anachokichimba.


"Ili bei iweze kupanda tunaomba tutengenezewe mfumo wa kupata nguvu ya uchumi katika mfuko itakayo tuwezesha kuuza madini kwa bei ambayo haitukandamizi."walisistiza wachimbaji hao


Wameongeza kuwa changamoto nyingine inayoeakabili wachimbaji hao ni ukosefu wa mitaji kwa baadhi yao ambapo aliomba kufahamu kuwa serikali imajipangaje katika kuhakikisha inamsaidia mchimbaji wa madini ya tanzanite.


"Zamani tulikuwa tunasaidia wote kwa pamoja lakini sasa hivi wachimbaji wamebaki wenyewe,auze shamba ndiyo apate hela ya kuchimba hivyo tunaomba tupate ruzuku ya zana za milipuko kutoka serikalini".waliongeza wachimbaji hao


Vilevile wameomba kupata ufafanuzi juu ya madini ambayo wanayapata kwani yamekuwa yakihifadhiwa na serikali baada ya kuthaminishwa na kukosekana mteja wa kuyanunua.


"Tunachimba mawe yanafanyiwa tathimini tunapeleka sokoni yasiponunuliwa tunaambiwa tuyaeudiseha sasa hapo sisi kama wachimbaji hatujapata maelezo ya kutosha kutoka wizarani kuwa madini hayo ni yetu au niya serikali."walieleza

No comments:

Post a Comment