Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo akiongea na wavuvi wa bwawa la mtera lililopo wilaya ya Iringa.

Na Fredy Mgunda,Iringa.

Wavuvi 12 wamepoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa katika kipindi cha mwezi wa pili 2020 hadi mwezi wa nane 2021 kufuatia matukio ya kuvamiwa na mnyama kiboko wakiwa ndani ya Bwawa hilo katika shughuli zao za uvuvi.

Hayo yamezungumzwa katika Ziara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ya kukagua Jitihada za Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA za kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali amewataka wavuvi kuzingatia njia sahihi za uvuvi salama ili kujilinda

Moyo alibainisha kuwa miongoni mwa sababu za matukio hayo yalioondosha uhai ni pamoja na shughuli za Uvuvi kufanyika kwenye mazizi ya viboko,tabia ya wavuvi kutumia zana dunu za uvuvi,kupungua kwa samaki katika bwawa hilo na wavuvi kufanya shughuli ya uvuvi nyakati za usiku ambapo viboko wanakuwa katika harakati za kutoka nje kutafuta chakula.

Moyo aliyetembelea Bwawa la Mtera katika ziara ya kukagua jitihada za Ziara yake ya kukagua Jitihada za Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA za kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali wakiwemo Viboko Na Tembo ameeleza kusikitishwa na matukio hayo huku akitaja miongoni mwa sababu zinazochochea kuwapo kwa hatari dhidi ya wavuvi.

Aidha Moyo Amewaagiza maafisa Uvuvi, viongozi wa Serikali kwa ngazi zote kusimamia na  kuhamasisha  njia bora za uvuvi katika Bwawa la Mtera  ili kuepuka migongano ya Wanyama pori wakali na waharibifu akisisitiza kufuata miongozo na kanuni za uvuvi

Lakini pia Moyo alisikitiswa na vifo vya wafugaji watatu wanaoishi ndani ya hifadhi ya pori tengefu la Lunda Mkwambi vilivyosababishwa na Tembo  wakati wakipita katika pori hilo la tukio hilo limekuwa kubwa kuwahi kutokea katika wilaya hiyo.

Alisema kuwa kuongezeka kwa mtawanyiko wa tembo katika eneo la hifadhi ya Pori tengefu Lunda Mkwambi na wafugaji kuishi porini humo na familia zao kunasababisha hatari ya maisha yao kwa kuwa wanaishi mahali ambapo sio salama kwa maisha yao.

Wakitoa kero zao miongoni mwa wavuvi wameeleza kuwa miongoni mwa sababu za kuendelea kuwapo kwa matukio ya kuvamiwa na viboko ni ongezeko la wanayama hao katika bwawa hilo ambao wamekuwa kero kwa wavuvi wa samaki katika bwawa la Mtera.

Walisema kuwa wanaiomba serikali kuhakikisha wanawavuna viboko hao mara kwa mara ili kupunguza vifo na majeruhi yanatokana na kuvamiwa na mnyama boko ambaye amekuwa tisho kwa maisha ya wavuvi ambao wanafanya shughuli ya uvuvi katika bwawa hilo.

Waliomba serikali kuakikisha wanaweka mbele maslai ya wananchi kwa kuwa ndio wanaojenga nchi kwa shughuli za kiuchumi ambazo wamekuwa wakizifanya katika bwawa hilo la Mtera.

Akitolea ufafanuzi juu ya malalamiko ya baadhi ya wavuvi Kamanda wa Uhifadhi Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA Nyanda za juu kusini Joas Makwati alisema kuwa hawezi kuvuna viboko wote bali kuna sheria na taratibu zinazowaongoza katika kuwavuna boko hao.

Alisema kuwa hivyo wavuvi wanatakiwa kutambua kuwa viboko wote wanaovunwa katika bwawa la Mtera huuzwa kwenye mabucha mbalimbali kwa ajili ya kitoweo kwa wananchi kwa mjibu wa taratibu na sheria za nchi zinavyotaka.

Makwati alisemuwa kuwa kwa mujibu wa Sensa iliyofanywa na Taasisi ya utafiti wa wanyama Pori Tanzania TAWIRI, Mwaka 2020 ilibaini kuwa bwawa hili linakadiriwa kuwa na voboko 261 sawa na asilimia 24 chini ya ustahimilivu wa Bwawa wa viboko 1070.

 Aliongeza kwa kusema kuwa kwa mujibu wa taratibu za TAWA za kudhibiti wanyama wakali na waharibifu unaendelea kufanyika katika bwawa la mtera ambapo tangu mwezi wa pili 2020 hadi mwezi wa nane 2021 jumla ya viboko 19 wamedhibitiwa kwa kuuwawa na kusaidia kupunguza kadhia inayowapata wavuvi wanapofanya shughuli za uvuvi bwawani huo.

Makwati alisema kwa licha ya changamoto hizo TAWA wamejipanga kuhakikisha wanaleta boti kwa ajili ya kuweka kambi na kikosi cha kudumu Lunda mkwambi ili kuwa na muitikio wa haraka pindi matukio hatarishi yanapojitokeza.

Alimalizia kwa kusema kuwa TAWA inaendelea kutoa elimu ya uhifadhi na njia za kuepukana na migongano kati ya binadam na wanayamapori hao wakiwepo tembo na viboko.

Bwawa la Mtera lenye ukubwa wa kilometa za mraba 660 linapatikana ndani ya halmashauri za wilaya tatu, halmashauri ya wilaya Iringa, na upande wa MKOA WA Dodoma lipo katika halmashauri ya Mpwapwa na chamwino

Share To:

Post A Comment: