Friday, 24 September 2021

Wakurugenzi Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato

 

Na. Angela Msimbira TAMISEMI


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. ummymwalimu amesema Wakurugenzi wa Halmashauri kupimwa kwa kigezo cha ukusanyaji wa mapato ya ndani na kutenga fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo inayotatua kero za wananchi. 


Akifungua Mafunzo ya Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa leo jijini Dodoma Waziri Ummy ameendelea kusema kuwa agenda ya mapato inaenda sambamba na kigezo cha kupima kiasi cha fedha kilichotolewa na Halmashauri katika kutatua kero za wananchi hususani katika miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya elimu, afya, barabara, Masoko, na kuwekeza kiuchumi wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.


Waziri Ummy amewataka kuhakikisha wanatenga asilimia 40 ya mapato  ya ndani yasiyolindwa inatengwa kwa ajili ya miradi ya maendeleo kwa Halmashauri ambazo zinapata mapato chini  ya Bilioni 5 na wale wanaokusanya zaidi ya bilioni tano wanatakiwa kutenga  asilimia 60


Anaendelea kusema kuwa Halmashauri nyingi zinatenga fedha lakini bado hazigusia moja kwa moja wananchi  kutatua kero za wananchi , niwaagize kuwa fedha hizo zisitumike  kwa matumizi  ya kuendesha ofisi  bali zitumike katika miradi ya maendeleo


“Sitegemei kuona fedha hizi zinatumika kwa ajili ya matumizi ya ofisi, nategemea fedha hizi zijenge zahanati, madarasa, mabweni, maabara, barabara, masoko, stendi na si kugharamia posho za vikao” amesisitiza Waziri Ummy 


Amewaagiza wakurugenzi kuhakikisha wanatumia mapato ya ndani kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendelo katika Halmashauri zao lengo likiwa ni kutatua kero za wananchi katika maeneo yao


Aidha amesema kuwa mapato na matumizi kwa maendeleo ya wananchi si kazi nyingine

No comments:

Post a Comment