Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.

Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.


Mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Prof. Ninatubu Lema,akizungumza wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.


Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,(hayupo pichani) wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki mara baada ya kufunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga,akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini yaliyofanyika jijini Dodoma ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.

.......................................................................................

Na.Alex Sonna,Dodoma

Serikali imewataka wahandisi wote nchini kuendelea kujisajili chini ya Bodi ya usajili wa Wahandisi Tanzania (ERB) ili waweze kutambulika kitaifa na kimataifa .

Kauli hiyo imetolewa jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga wakati akifunga maadhimisho ya 18 ya siku ya wahandisi nchini ambapo zaidi ya Wahandisi 3000 walihudhuria huku Wahandisi 630 wakila kiapo.


Mhandisi Sanga amesema kuwa kujisajili kwa wahandisi ni takwa la kisheria hivyo mlango uko wazi kwa kila mhandisi kujisajili huku akihimiza kwa wahitimu fani ya uhandisi kutoka vyuo mbalimbali kuchangamkia fursa hiyo.


''kufanya hivyo itasaidia zaidi wahandisi kuaminika kitaifa na kimataifa zaidi pamoja na kuepusha watu wanaofanya kazi ya uhandisi kutekeleza miradi ya miundombinu licha ya kuwa hawana vigezo hali ambayo husababisha miradi kutekelezwa kwa kiwango cha chini''amesema Mhandisi Sanga

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya wahandisi, Prof. Ninatubu Lema, amesema zaidi ya watu 800 wamefuatilia kwa njia ya mtandao hivyo idadi ya watu wote waliofuatilia ikiwa ni zaidi ya 3700 ikivuka lengo ambapo matarajio ilikuwa ni watu 3200.


Naye Msajili wa Bodi ya Wahandisi Patric Barozi, amesema kuwa siku tatu kulihusishwa mijadala ya kitaaluma,Maonesho ya Ubunifu,Sayansi na Teknolojia huku pia Makampuni 61 yakishiriki.
Share To:

JOHN BUKUKU

Post A Comment: