SHIRIKISHO la Wanafunzi wa Vyuo vya Elimu ya Juu nchini (TAHLISO)linatarajia kukutana na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya nchini(NHIF)  kwa lengo la kutatua changamoto mbalimbali za upatikanaji wa bima za afya kwa wanafunzi ambazo kwa nyakati fofauti wamekuwa wakizilalamikia.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamishina wa Afya na Mazingira  wa Tahliso Sospeter  Bulugu kikao hicho kinachotarajiwa kufanyika Septemba 13 Mwaka huu, pamoja na mambo mengine kitatoa majibu ya kina dhidi ya malalamiko hayo ambayo amedai kuwa yamekuwepo kwa muda mrefu.

“Nitumie nafasi hii kuwapongeza wale wote ambao muda mwingi  wamekuwa wakilifuatilia suala hili kwa lengo la kujua hatua zimefikia wapi, kimsingi malalamiko kuhusu suala la bima ya afya yamekuwa maumivu ya kujirudia rudia imani yetu kikao hicho kitatoa muafaka wa changamoto hizo” alisema Bulugu

Alisema mbali na hayo, kikao hicho pia  hususani kwa upande wa Tahliso kinatarajiwa kupata mrejesho wa mambo mbalimbali ambayo pande hizo mbili zilijadiriana na ili kuona njia nyingine inayoweza kutoa majibu kwa yale mambo ambayo wanaoona bado hayajafanyiwa kazi.

Aidha Bulugu alisema mapendekezo aliyowahi kuyasilisha ili kutatua changamoto ya upatikanaji wa bima ya afya kwa wanafunzi, ni pamoja na   kuishauri Serikali kutoa tamko  kwa kila Chuo Kuwa na msimamizi wa masuala ya afya na bima hatua itakayomfanya kuwa na kanzidata  za wanafunzi wote kuhusu taarifa za bima ili kuondoa mkanganyiko.

“Hatua hii itatusaidia kujua changamoto ipo wapi,na nani mzembe..kwa kufanya hivyo naamini tatizo litaweza kutambulika mapema na kufanyiwa kazi kwa kuwa kutakuwa na ushirikiano wa moja kwa moja kati ya afisa huyo na mwanafunzi” aliongeza Bulugu

Share To:

Post A Comment: