Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imedhamiria kuendesha sekta ya Sanaa kibiashara na kuongeza tija ikiwa ni pamoja na kuwezesha sekta hii kutumika kama nyenzo ya kuhamasisha na kuelimisha jamii kuhusu masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe Septemba 29, 2021 wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Sekta ya Sanaa 2021 ambao lengo lake ni kujadili kwa Pamoja masuala yanayohusu Sekta ya Sanaa kati ya Serikali na wadau ili kufikia lengo la kuifanya sekta hii kuendeshwa kibiashara ambapo kauli mbiu ya mkutano huo ni “Sanaa Biashara”

“Serikali imejipanga kuweka mazingira wezeshi ya kukuza Sanaa zetu ili kufikia viwango vya kimataifa na kuboresha mbinu na Mikakati ya Utekelezaji wa sera na Sheria za kuimalisha kazi za Sanaa nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Sanaa hususani wasanii” amaeeleza Mhe. Exaud Kigahe

Aidha, Mhe. Exaud Kigahe ameeleza kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara ni mdau mkubwa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo kwani Sekta ya Sanaa ni kiwanda kinachozalisha bidhaa na huduma za sanaa ambazo zinahitaji mchango mkubwa wa Wizara ya Viwanda na Biashara katika kuweka sera, sheria, kanuni na miongozo mbalimbali ya kusimamia uendeshaji wake na kuiendeleza kama inavyofanyika katika Sekta nyingine za kiuchumi hapa nchini.

Kwa upande wake, Dkt. Emmanuel Ishengoma Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaaa wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo ameeleza kuwa ili kuendesha Sanaa kibiashara, Serikali imeanzisha mfuko wa Utamaduni na Sanaa ambao utasaidia kuimarisha sekta hiyo kwa kudhamini mafunzo vilevile kutoa mkopo kwa mashariti nafuu ya kusaidia Sanaa na utamaduni na mpaka sasa Serikali imeshatoa billioni moja na milioni mia tano za kuwezesha mfuko huo.
Share To:

emmanuel mbatilo

Post A Comment: