Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (Mb) ametoa wiki mbili kwa Meneja wa Maji Mkoa wa Njombe (RUWASA) Mhandisi Sadick Chakka kuhakikisha tatizo la uvujaji wa maji katika tenki la kijiji cha Usililo wilayani Makete linapatiwa ufumbuzi.


Agizo hilo amelitoa jana Septemba 27, 2021 baada ya kukagua na kubaini kuwa tanki hilo linavuja hali ambayo inasababisha kupungua kiwango cha maji yanayokusudiwa kuwafikia wananchi.


"Meneja wa RUWASA mkoa, hili lipo ndani ya uwezo wako. Nakupa wiki mbili hili tatizo liwe limemalizika. Taarifa inaeleza kuwa kuna upungufu wa maji, halafu hayo yanayopatikana kidogo bado yanavuja. Hili tatizo limalizike haraka." Amesema Mhe. Mahundi


Aidha, Mhe. Mahundi amewaambia wananchi wa kata ya Luwumbu katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha  Usililo kuwa serikali imesikia kilio chao na kutoa fedha ambazo zitaanza kutatua kero ya maji katika vijiji vya kata hiyo.


Naibu Waziri. Mhe. Mahundi yuko ziara ya kikazi mkoani Njombe kwa lengo la kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.

Share To:

Post A Comment: