Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl.Zainabu Makwinya ameziagiza kamati za ujenzi wa Miradi ya lipa kutokana na matokeo EP4R kuhakikisha  miradi ya vyumba vya Madarasa na mabweni  pamoja na miradi ya vyoo vya muundo wa SWASH inakamilika kwa wakati na uimara mkubwa.

Aidha Mwl.Makwinya amewataka mafundi wanaotekeleza miradi hiyo kuongeza nguvu kazi ili  kukamilisha miradi hiyo kwa wakati na bila kuathiri ubora"kuongeza idadi ya mafundi haiongezi gharama, hupunguza siku za kufanya Kazi kwani kazi ya siku kumi ikifanywa na mafundi nane badala ya wanne itakuwa ya siku tano" ahimiza Makwinya

Mwl.Makwinya amesema amefanya ziara hiyo kuona uhalisia wa Miradi hiyo ambayo Serikali ilitoa zaidi ya Milioni  480 ambayo ilitakiwa kukamilika Juni 30 ambapo amehimiza uzalendo ni muhimu katika Kutekeleza miradi hiyo.

Aidha Miradi iliyotembelewa ni    Ujenzi wa Bweni moja na vyumba vya madarasa viwili Shule ya Sekondari Mbuguni, Ujenzi wa  Bweni moja Shule ya Sekondari Maroroni, Ujenzi wa Bweni moja Shule ya Sekondari Kikwe,  ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ujenzi wa matundu Kumi ya vyoo ya wanafunzi na matundu mawili ya walimu Shule ya Sekondari Akeri,ujenzi wa vyoo matundu 12 shule ya Sekondari Lakitatu,Ujenzi wa madarasa 2 shule ya Msingi Kilimani,Ujenzi wa Vyoo matundu 12 shule ya Msingi Uraki.

Ikumbukwe Mkurugenzi Zainabu aliagiza miradi yote ya  P4R na Vyoo vya muundo wa SWASH kukamilika ifikapo tarehe 30 Septemba 2021.Share To:

Post A Comment: