Sunday, 26 September 2021

CCM ARUSHA WAMPONGEZA RAIS SAMIA.


 


Na Mwandishi wetu,Arusha.


CHAMA Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Arusha kimempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa chama hicho,Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuwaletea wananchi maendeleo na kuitangaza Tanzania kiuchumi.

Akitoa Tamko la Kikao cha Halmashauri kuu ya CCM kilichofanyika Septemba 24 mwaka huu,Mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Arusha,Zelothe Stephene alisema pamoja na mambo mengine chama kinampongeza kwa kazi kubwa anayoifanya.

Zelothe alisema pia Halmashauri kuu ya CCM mkoa inaunga mkono kauli aliyoitoa rais Samia siku ya Demokrasia Duniani ambayo aliweka wazi dhamira yake ya mwaka 2025

“Kwa ujumla tunaungana na watanzania wenzetu katika kumsaidia kufanya kazi  kwa bidii ili kuendelea kuimarisha uchumi wan chi yetu,kutoa huduma kwa watanzania na kuendelea kuimarisha mahusiano na nchi nyingine.”

Mwenyekiti huyo wa mkoa alisema pia Halmashauri kuu mkoa inawasisitiza wanaCCM na wananchi hususani wa mkoa huo kuendelea kujikinga na Ugonjwa wa Covid-19 ikiwa ni pamoja na kusikiliza ushauri wa wataalamu wa afya kutumia vitakasa mikono,kuvaa barakoa kwenye mikusanyiko na kwenda kupata chanjo.

“Pia tunampongeza Mhe Rais  kwa kuhutubia kwa mara ya kwanza Baraza kuu la Umoja wa Mataifa na kuihakikishia Jumuia ya kimataifa kuwa katika uongozi wake Tanzania itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na mataifa ya nje na wadau wengine Duniani.” Aliongeza Zelothe.

Zelothe pia Rrais katika hotuba hiyo  alizungumzia changamoto ya ugonjwa wa Corona  na jinsi unavyosumbua Dunia na akazishukuru Taaisis mbalimbali za kimataifa kwa jinsi zinavyopambana na ugonjwa huo na akazihakikishia kuwa Tanzania haitokuwa nyuma katika jitihada hizo.

Alisema pi Halmashauri kuu ya mkoa ilifurahishwa rais kueleza jitihada za Serikali ya Tanzania katika kuongeza ushiriki wa wanawake katika Nyanja za kiuchumi ikiwa ni pamoja na kuweka sera madhubuti na maboresho  ya mfumo wa kibajeti ili kupunguza idadi ya wanawake na wasichana waishio katika lindi la umasikini.

Pongezi nyingine ki kutokana na rais kuzungumzia athari za mabadiliko ya tabia ya nchi na umuhimu wa kuchukua hatua za kukabiliana na janga hilo na kuyasisitiza Mataifa yaliyoendelea kutimiza makubaliano yao ya Azimio la Paris.

“Sisis Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Arusha tunamuunga mkono Mhe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan kwa uthubutu na uongozi wake madhubuti na tunaamini yutasimama na yeye.” Alisisitiza.No comments:

Post a Comment