Wednesday, 18 August 2021

WALAFI WA FEDHA ZA TASAF WAONYWA, JELA MIAKA SABA INAWAHUSU

 


Mstahiki Meya manispaa ya Moshi Juma Raibu leo amewatembelea wanufaika wa mpango wa tatu wa Tasaf kwa kaya masikini.


Akizungumza katika hafla hiyo Meya Raibu amewataka viongozi wa Tasaf Na waratibu Wote kusimamia haki Ili wahusika halisi wa kaya hizo wapate fursa hiyo bila upendeleo lakini pia amewataka wananchi kuwabaini watu wote wasiojiweza na kuwaumbua wanaojiweza Ili Fedha hizo ziende Kwa walengwa wa kaya hizo kama lilivyo agizo La Rais Samia Suluhu Hasan.

*"Wako baadhi ya viongozi na watu wenye uwezo wanajiweka hapa kupata hii fursa, naomba niseme ni marufuku na nikibaini wote wanaenda Jela  miaka Saba"alisema Raibu


Endeleeni kumuunga na kumuombea Rais Samia Suluhu na Serikali yake Ili mambo haya yaendelee kuwa ya uwazi na ukweli kama mnavyoona sasa na ninyi wananchi ndio mnajuana watajeni wasiotakiwa kupata fedha hizi bila woga Ili Fedha Zenu zisikwapuliwe na walafi wachache wenye Nia ovu.


No comments:

Post a Comment