Friday, 20 August 2021

TAMISEMI kupokea Sh. Bil. 37. 5 za Tozo ya Mawasiliano; Itajenga Vituo vya Afya 150
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI


Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa @ortamisemitz imeanza kupokea Tsh Bil 22 kutoka Wizara ya Fedha na Mipango zitokanazo na tozo ya Mawasiliano na fedha hizo zinakwenda kujenga vituo vya Afya 90 kwenye Halmashauri 82 Nchini.


 Fedha hizo zimepelekwa kwenye Maeneo ambayo hayana kabisa Kituo cha  Afya kwenye Tarafa 90 kati ya 207 ambazo hazina kituo cha Afya kabisa.


Aidha  Shilingi. Bil 15 zitakazopokelewa juma liljalo kutoka Wizara ya Fedha ambazo zitapelekwa kujengwa Vituo vya Afya 60 hivyo kufanya Jumla ya Vituo 150 kujengwa kupitia Tozo ya mawasiliano.


Fedha hizi zinaKwenda na maelekeoz maalumu kuwa Vituo vya Afya vijengwe kwenye Tarafa ambazo hazina vituo vya Afya au vilivyopo havina uwezo wa kufanya upasuaji wa dharura.


Tanzania bara tuna jumla ya Tarafa 570 na mpaka hivi sasa Tarafa 207 hazina Vituo vya Afya hivyo kutokana na fedha za Tozo ya Mawasiliano tutajenga Vituo vya Afya kwenye Tarafa  150 na kubakia na Tarafa 57 tu ambazo zitakua hazina vituo vya Afya.

No comments:

Post a Comment